Nimeanza kuonja madai ya walimu

Afande Fojuman

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
657
Reaction score
548
Hi,

Mimi ni kijana na mwajiliwa mpya katika tasnia hii pendwa ya Ualimu,

Baada ya kupata post ya kuchaguliwa na TAMISEMI nilifurahi sana na kuandaa ATP kama zote ili kuendana na Kasi ya JPM.

Tangu niripoti kituoni ni takribani wiki sita sasa na hatujapewa Hela ya kujikimu wala mshahara na kupelekea maisha kuwa magumu hali inayopelekea kushusha motisha ya kazi mapemaaaa.

Kila Tukienda halmashauri tunapewa maneno ya kutufariji na kutuomba tuwe wavumilivu.

Nilikuaga nasikia tu redioni madai ya walimu tokea nipo mdogo ila leo naanza kujionea live.

Wahusika Tunaomba mtusaidie maana hali mi tete.
 
Hii kazi me naonaga Kama ina nuksi fulani ukiwa teacher ni bahati Sana kutajirika.home kwetu wote walimu nilivomalizaga shule walitaka nichague vyuo vya ualimu niligoma asee.ila Bora ningeendaga hata huo ualimu nibembeleze hivyo vi laki tatu maana huku nilipo ndo majanga zaid.niishie hapa
 
Ungechagua tu ualimu mkuu, maana uku at least bado tuna ajiriwa
 
Kuna wale vijana walikuwaga wanasoma petroleum,leo hii wanasugua gaga tu
 
uwalimu ni wito kijana wewe hizo wiki chache tu ushaanza kulia wenzako wana miaka 10 wanadai tu n
 
Wajaribu nje UAE watatoboa,wafilipino,wapakistan,wanatoka sana nje kutafuta Pesa kuja kuwekeza kwao sie tumelala sana,wachwa tusomeshwe no.Ajira tele nje.
Kuna wale vijana walikuwaga wanasoma petroleum,leo hii wanasugua gaga tu
 
Uko ulipo unalìpwa buku 7 tu
 
Bila picha,hainogi
 
Nena mkuu huko uliko ni wapi,na kuna majanga gani!

Maana nina dogo langu Fulani hapa,linanisumbua sana nataka nilitafutie course ya kwenda kusoma!

Kupitia wewe naweza epuka kumpeleka hapo ulipo wewe!
 
Ulikuwa huamini?? Picha kamili bado kuwa mvumilivu
 
Ndo unatakiwa ujue unapoona wengine wanapigia kelele jambo fulani usidharau nakudhani madhara yake wewe hayatakukuta.Hapo ilichagua mwenyewe nakuipenda mwenyewe pambana.
 
Mbona km nmekuona unaenda kumuona mkurugenz wa Magu alafu ukakuta anakaimu afsa utumishi mlikuwa wawili ila wafupi
 
mkuu wako wa shule hajakugawia kale kaposho wanakopata kila mwezi?
 
Maisha yana Falsafa pana sn.....komaa ndugu pia vuta subira mana kisichokusaidia Leo kitakusaidia kesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…