Anselm
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 1,710
- 291
Leo ngoja niibukie kivingine kidogo,nafikiri kwenye ukweli wacha tuongee ukweli,kuna kila dalili kuwa Watani zetu (Simba S.C) wamelamba dume kwa usajili wao walioufanya dakika za lala salama hasa mshambuliaji Mghana Daniel Akuffor,binafsi sijawahi kumshuhudia akicheza lkn record yake ya upachikaji mabao kama ambavyo nimekuwa nikiisoma kwenye vyombo vya habari vinavyo'report mwenendo wa maandalizi ya Watani zetu kule Arusha ni dhahiri kabisa he is by far better than Sunzu, wakati Sunzu anaweza kucheza mechi 10 kama Simba isipopata penalt akapewa apige anaweza kuzimaliza bila kufunga hata goli 1,Akuffor yeye katika mechi 4 za kirafiki ambazo ameshaichezea Simba ametupia mechi 3,hii ni dalili nzuri kwa Mshambuliaji, he even looks better than Kavumbagu wetu but he will need to work hard to be better than Mzawa wetu Side Bahanuzi "Spiderman".