Nimeamu kuoa Kenya,kama Ali Kiba

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
NAKUJA KUOA KENYA

1)Acha niseme ukweli,nitue huu mzigo
Naende kuoa mbali,huku nakupa kidogo
Nawabwaga chini chalk,nashusha yangu mapigo
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.


2)Huku wengi omba omba,wanapenda kutuchuna
Wanapenda omba omba,kwa hilo ninawachana
Japokuwa wapo bomba,ila upendo hakuna.
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.


3)Wabongo waringa sana,wataka mahari kubwa
Wanapenda vilivyonona,kuku baga na ubwabwa
Kwa mahari washindana,shindwa wakwone jibwa
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.


4)Wanaweza kutajia,mahari mamilioni
Kama wanatukomoa,twajifanya hatuoni
Kenya nakuja kuoa,make nimpe thamani
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.





5)Hawana penzi la kweli,huku wanawaza pesa
Jitie we ujahili,uone watakutesa
Nakuja kuoa mbali,bila jicho kupepesa
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.


6)Sura zao za dukani,tena ghali waziuza
Najitoa mashakani,sitaki mauza uza
Wajiona wa thamani,na utu waupuuza
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.


7)Nimechagu wakenya,wanaojua kulea
Namanga ninaipenya,Nairobi.nasogea
Watanga ninawaonya,wamrshaji haribia.
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.

8)Bongo wanaringa ringa,na midomo wabenua
Nakipuliza kipenga,ili kesho waje kua.
Wametupa ya wahenga,yuropa wamechukua
Nakuja kuoa Kenya,wabongo wamenishinda.


SHAIRI-NAKUJA KUOA KENYA
MTUNZI-Idd Ninga,Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom