Ni ukweli usiopingika, kwamba hii vita ni ngumu. Tuhuma zote sasa zinamuendea mtu mmoja na ukiangalia kwa undani kwa namna moja ama nyingine wote wanaopeleka mashambulizi kwa huyo mtu ni kwamba kama hajaguswa yy basi ni mtu wa karibu yake. Imefika mahali sasa mjadala umehamia kwenye maisha yake binafsi, nashindwa kupata picha hata kiongozi wa kiroho ndg Gwaname nae kaamua kulipa kisasi kwa kumchafua yule ndugu kuwa ana vyeti fake, na ni huyu huyu Gwaname alimtukana Pengo, na kwa busara za Pengo wala hamkujibu, Gwaname ww ni kiongozi wa dini kweli ? Kuna haja yakuacha kufuatilia maisha binafsi ya mtu, bali tujikite na yale ya msingi