Nimeachwa njia panda

hahaha madhara ya kuwa niceguy utvurugwa mpaka ujezinduka umegeuka zombi nikushauri never kiss women ass....
 
Nisingeweza kumuona kwa kipindi hicho maana alikua bado anasoma na mimi ndo nilikua naanza mbio za kutafuta maisha. Na miaka saba ni tulianza kama marafiki tukawa wapenzi na mwaka jana tukawa wachumba rasmi
 
hahaha madhara ya kuwa niceguy utvurugwa mpaka ujezinduka umegeuka zombi nikushauri never kiss women ass....
Sio wanawake wote wako hivyo. Kuna wanawake na wasichana wanajiheshimu sana. Baada ya kuwa nae kwa kipindi kirefu sio mimi tu hata ndugu na marafiki walikua wanasema nimshirikishe tu kwa kila kitu. I still doesn't know what happen to her.
 
Mkuu justin kwanza sio story ya kuondolea stress ni ukweli yaliyonikuta wala sikusikia kwa mtu ni mimi mwenyewe niliyepatwa na hili tatizo.
2 suara la hela mshahara wangu uko juu kidogo ya la 9 na nilikua namtumia hizo hela kwa ajili ya maendeleo yetu na matumizi yake madogo madogo ilipokua inaitajika hela ndefu kama ya kujengea nilikua namtumia pia. Kwa asilimia nyingi alishakua kama mke wangu bado tu kuhararisha kwa ndoa sikua na haraka ya kuzaa kiivyo ila tuliongea na kukubaliana
Suara la kungojea ilikua ni kujipanga tu kimaisha na yeye amalize shule kwanza.
Kwa lolote litakalotokea nakuahaidi siwezi kua kama mushi. Nitatafuta hela na nitafanya mazuri na nitamwomba mungu nipate mke mwema
 
Aisee, hongera sana kwa kupenda, Ila hapo ndio ulipofanya makosa. Mimi huwa nasema siwezi kumwamini mwanamke yeyote isipokuwa mama yangu tu.
Ukipata mwanamke unayempenda jaribu kumwamini tu ndugu yangu. Ni kosa kama unajua tabia yake lakini kama hujui sio kosa hata kidogo. Hata hivyo nimekuelewa sana tu na shukurani sana
 
cha muhimu mpigie simu doctor aliyempima hyo mimba akueleze ukwel namba za doctor mwombe yule ndgu ako aliyewah kumsindikiz klinic atakutafutia
 
Bandu bandu. Kweli tulizini kabla ya ndoa ni zambi nakubali lakini ndo maana kukawa na zambi ili tuweze kutubu nitajie mtu mmoja unayemjua ambaye hajawai kufanya zambi au dhambi kwako ni mapenzi tu?
 
Mkuu nakumbuka stori yako kuna wakati ulieleza hapa nadhani zilikuwa ni habari za clinic...

Tofauti na watu wengine walioonesha wasiwasi mimi kidogo napingana na mawazo yao...

Sidhani kama ni sahihi kwa wewe kuanza kumtilia shaka mkeo mtarajiwa kuwa anakudanganya...

Umeeleza wazi kabisa kuwa huwa una kawaida ya kumtumia pesa ya matumizi mara kwa mara.

Naamini umekuwa ukifanya hivyo pasipo shinikizo toka kwa mtu yoyote bali ni mapenzi yako kwa mkeo mtarajiwa.

Kama ingelikuwa huyo dada anatumia mimba kama chambo cha kuvuna pesa toka kwako, basi tabia kama hiyo ya uroho wa pesa ungeiona huko mwanzoni kwa mbinu nyinginezo.

Mimi naamini huyo dada hakutaka kukuumiza baada ya kupata miscarriage ndio maana ilimchukua muda kuweza kukupa ukweli wa mambo.

Ukiaanza kujawa na mawazo hasi juu ya mkeo mtarajiwa ujue huo ndio mwanzo wa kukaribisha ukosefu wa furaha kwenye mahusiano yenu.

Labda nikuulize swali moja, Je wakwe au wazazi zako walikuwa wana taarifa kuwa mchumba wako ni mjamzito?
 
Jestina ni mapenzi tu ndugu yangu nilimpenda sana na bado nampenda ingawa sitakuja kumwamini tena
Massa kama umefikia hapo, cha kufanya njoo nyumbani mara moja sort it out, ikijumuisha kutafuta ushahidi halisi wa hiyo mimba nk, then fanya uamuzi wa kuendela au kuachana naye kulingana na hali utakavoikuta. zingatia sana ushauri wa watu hapa maana naona dalili zote za kutupiwa mchanga wa macho kwa mujibu wa maelezo yako. usiangalie sana kigezo cha muda u may find the right one in no time
 
Last edited by a moderator:
Watu8
Aksante sana kwa ushauri ndugu yangu. Ni kweli kwa kipindi chote cha uhusiano wetu hakuwai kua na tabia ya kuomba hela kwa kisingizio chochote na alikua yuko karibu sana na familia yangu kiasi kwamba hela nyingi nilizokua namtumia kwa matumizi basi yeye alikua anatumia kuwapa watu wa nyumbani kwetu. Nilikua hadi namgombeza kuhusu hiyo tabia. Nilisha waambia nyumbani mwenye shida basi awasiliane na mimi na sijisifii sijawai kutokumsaidia ndugu pale napo weza

Suara la kutokutaka kuniumiza inawezekana ni kweli lakini sikuona sababu ya kwa nini asiniambie tu mapema ikizingatiwa na wachumba.

Nilipata kuongea na mama yake akanisibitishia kua alikua na mimba na kweli ilitoka. Kwa upande wa kwetu sina wazazi wote walishatangulia mbele ya haki hila ndugu zangu wote walikua wanajua anamimba. Kaka yangu mkubwa alimuona na akahisi kitu akamuuliza akakubali kua anamimba

Mambo mengine nazani itabidi nimuulize tu vizuri nikija huko lakini rohoni nina kinyongo na maswali mengi kuliko majibu.
 
Umenijibu vyema sana na umenipa maelezo niliyokuwa nayahitaji kutoka kwako...

Ni hivi ndugu yangu wasiwasi ulionao ndio unaokuweka katika fikra ulizonazo sasa...Ni wakati sasa inabidi uamini kuwa mpenzi wako alikuwa anajaribu kulinda furaha yako wakati akijipanga namna ya kukueleza.

Huenda hata suala la kuchelewa kukueleza halikuwa ni muono wake bali ilikuwa ni baada ya kupata shauri toka kwa watu wa karibu pengine kuepuka wasije kukuchanganya huko ng'ambo ulipo...

Huu sio wakati wa kumchanganya zaidi huyo mpenzi wako, ni muda wa kuwa naye karibu zaidi na kumpa faraja.

Ningelikuwa nina wasiwasi sana kama ndugu zako au wazazi wake hawatambui kama mchumba wako alikuwa na ujauzito.

 

"Miaka 10 away from home" hapo huna mchumba. Maisha ya siku hizi kitu cha kurudia nyumbani ni documents tu, wanawake wapo kila sehemu.
 
Hyuo yawezekana aliiporomosha muda mrefu sana...

Cha muhimu ni kuomba vyeti vya hospitali(clinic) alipokua anakwenda
 

wewe kweli pi*bi. Utamshirikishaje mwanamke ambaye hujafunga nae ndoa katika maswala makubwa kama hayo? Kwa taarifa yako, hizo fedha ulizokuwa ukimtumia kulea mimba na kufanya vimaendelo alikua anapaa nyoka na mtu aliyekuwa akimuhudumia yale mambo ya kwenye Bed wakati wewe eti "10 yrs away from home"
 


wajanja wa mjini wameshamuharibu huyo.............

huwezi kuka na mwanamke mbali hata kwa miezi sita (6) itakula kwenu siku zote.............

hapo kuna mengi sana huyajua, amini nikuambiayo.............
 
Bra-Joe mimi sio pimbi ndugu yangu hivi unazani waliofunga ndoa hadi kua na familia hawana matatizo?

Ni mara ngapi umewai kusikia jamaa kamfumania mke wake na wanakaa pamoja sio kama mwingine kasafiri.

Suala la kuluka nyoka mbona wapo wengi tu wameolewa na bado wanaluka nyoka na wanaume wengine.
Nilimwamini kwa kua nampenda
Niko nje ya nchi kutafuta ni maisha tu na siko peke yangu wapo wengi kama mimi. Karibu na wewe utafute au wewe wazazi wako ndo wanaibia watanzania wanakuletea zawadi za smartphone ndo unapata nafasi ya kuingia jf kutuka wenzio. Kua mwanaume na tafuta kama mimi na usione miaka 10 ni mingi kwenye kutafuta. Wapo watu wanamiaka 60 na bado wanatafuta. Asante kwa ushauri bro Joe
 
Nichukue mm nikupe pumziko la moyo..kwikwikwikwiiii
Asante mayasia usijali utampata mme mwema zaidi yangu mimi. Bado Sijui uhusiano wetu utakua vipi nikirudi na kuongea nae. Ukweli bado nampenda sana tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…