Nimeachwa njia panda

Massa

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
709
Reaction score
891
Habari zenu wakuu
Mwanzoni mwa mwaka huu niliomba ushauri kuhusu mchumba wangu kukataliwa kupewa huduma alipoenda klinik nilipata majibu mazuri sana kutoka kwa watu mbali mbali waliopata nafasi ya kujibu. Sasa kwa kipindi cha miezi kazaa nimekua mtu wa mawazo sana baada ya huyo mchumba wangu kunambia mimba ilitoka ikiwa na week 13 tatizo ni aliniambia tiari ikiwa ni miezi Sita toka aliponiambia anamimba. Kwa kipindi chote nilikua naongea nae kila siku kwa simu au Skype na alikua ananitumia picha kuona mabadiliko ya mwili kama tumbo na nilikua na uhakika wa yeye kua na mimba kwa kipindi chote hicho cha miezi sita. Siku aliponiambia hana mimba na ilitoka ikiwa na miezi mitatu kweli mungu ndiye anajua tu lakini niliuzunika kupita maelezo. Kwa sasa bado kichwani nina maswali ingawa nilishamuuliza zaidi ya mara 1000 kweli alikua na mimba au alikua ananiongopea na kama kweli ilitoka ikiwa miezi mitatu na week moja kwa nini alisubilia kipindi chote hicho bira kunambia? Kwao najulikana na kwetu wanamjua na suala la kuanza familia tulikubaliana wote. Week tatu zijazo nitakua tena likizo nyumbani huko na nashindwa nini cha kufanya kuhusu huyu mchumba wangu. Ushauri wenu ni wa muhimu sana kwangu naomba mnishauri nini nifanye japo kwa kuanzia nikikutana nae tena.
Angalizo kwa wote ni story ya kweli iliyonitokea mimi
 
Kwa sababu unaenda karibuni basi kaongee nae umuulize maswali yote yanayosumbua akili yako kwa sasa,maamuzi yatakayofata yatategemea majibu atakayokupa yatakuridhisha kiasi gani na mwisho wa siku mwamuzi wa mwisho ni mjeruhiwa moyo wako.
POLE.
 
Ukifika mwambie akupe magamba ya hospitali ili uthibitishe hiyo mimba iliharibikaje!
...
Mambo matatu 1 linawezekana:
1 Aliitoa makusudi!
2 Iliharibika bahati mbaya!
3 Hakuwa na mimba! Alikutumia tu picha baada ya kushiba ugali + kujibenua + kujivimbisha!
Miezi mitatu katumbo kanakua kadogo tu!
...
NB: usikurupuke muda huu kumuulizia hayo magamba ya hospitali!
 
Kwa sababu unaenda karibuni basi kaongee nae umuulize maswali yote yanayosumbua akili yako kwa sasa,maamuzi yatakayofata yatategemea majibu atakayokupa yatakuridhisha kiasi gani na mwisho wa siku mwamuzi wa mwisho ni mjeruhiwa moyo wako.
POLE.
Aksante Ennie nitamuuliza tena ingawa nilishamuuliza mara nyingi tu. Tatizo moyoni nashindwa hata kuhamua ilikua niache kazi moja kwa moja nije nianze maisha nyumbani lakini naona kama nitakuja kujutia uamzi wangu kama nitahamua kuacha. Hivyo nimeomba likizo ndefu kuja kuweka mambo sawa kwanza
 
Inasikitishaga beyond reasonable measure THE ONLY THING KEEPING YOUR GUY IS THE PREGGO/BABY!!!!!!!!! Inatia huruma!
 
hiyo namba moja kwa nini aitoe wakati tulikubaliana na ni official wachumba na mambo kibao nilikua nafanya kwa ajili yake na familia yetu. Sioni sababu ya maana hata kidogo.
2 kwanini asubili hadi baada ya miezi sita? Na je picha alizokua ananitumia nazo?
3 hiyo nawaza kama wewe swali kwake ni kwanini aseme anamimba wakati hana? Haikua lazima sana na nilimwambia asipokua na mimba tutajaribu tena nikija na ilikua nije moja kwa moja kuishi baada ya miaka 10 away from home
 
pole hapana chezea batoto ya mujini. anabeba mimba anasikilizia response kuhusiana na suala la huduma kagundua utamsumbua kwenye issue ya matunzo. jitahidi usiwe mkono wa birika
 
Inasikitishaga beyond reasonable measure THE ONLY THING KEEPING YOUR GUY IS THE PREGGO/BABY!!!!!!!!! Inatia huruma!
Sio kweli Lara 1 we've been together for over seven years na muda wote huo hakuna hata mara moja nilishamwambia au kumlazimisha kuzaa na mimi. Suala la kuanza familia tuliongea wote mimi na yeye na tulipata baraka kutoka pande zote za family. Kuanza familia. Jaribu kua unasoma vizuri post ndo useme hivyo. Sasa kama tulikubaliana kwa nini anidanganye? Ndo swali langu tafadhari Lara 1 be in my shoes and think what will you do if it happen to you
 
pole hapana chezea batoto ya mujini. anabeba mimba anasikilizia response kuhusiana na suala la huduma kagundua utamsumbua kwenye issue ya matunzo. jitahidi usiwe mkono wa birika
Sista nimefanya kila kizuri unachokijua mwanaume inabidi amfanyie mpenzi wake hadi nyumba inajengwa na kila kitu ni Jina lake. Kwa mwezi nilikua namtumia na bado namtumia si chini ya laki sita. Na tuko pamoja miaka 7 na nusu. What more can I do?
 
1.hakuwa wako despite kumuonyesha mapenzi ya kweli...hauko kichwani kwake/hamna future pamoja at least hamkuwa pamoja.learn to .move on .................
2.sioni sababu ya kudabnganya wkt ni wachumba rasmi, hivyo inawezekana ilitoka kweli
3,kuna couple zimeishi miaka kibao bila watoto...usipanie mno,you will get in no time,piga goti kwanza/sali mungu akuonyeshe namna ya kujinasua....mbele ya walaghai wa mapenzi,....
mwisho huko ulipokuwa kulikuwa hamna wadada au una 'aleji' na kutongoza:tape:a,dada kakuona una udhaifu huu na atakupelekesha ukimweka ndani na mauongo yake......

watu mnajiamini eeh uache kazi na sehemu uliyoishi zaidi ya mlongo mmoja kwa dada ambae future nae inaonyesha chenga?????
 
Kwani uko ichi gani Mura?
Hicho kiwekeo cha mimba si bado unacho? Ukija weka kabisa ila kama ungependa kumkuta mjamzito uweke picha yake na no. zake za simu vijana wa sirari wakurengee mura!
 
Yote anaejua ni Mungu Mkuu. Kama alikudandaganya kuwa ana mimba halafu ikatoka au kama aliitoa Mungu ndie anaejua. Kama atakuwa mke wako wa maisha Mungu ndie atakaepanga pia. Usichoke kumomba Mungu.
 
Labda nikupe mfano wa rafiki yangu fulani hivi anaishi mkoani Mwanza.

Alikuwa na mchumba wake huku Morogoro ambapo mimi nilikuwepo kipindi hicho. Basi ikawa mchumba anaendwa Mwanza kumtembelea then anarudi Morogoro. Huyu mchumba wake hatukuwa karibu sana. Ukaribu ulikuwa tu rafiki yangu akija Moro.

Baada ya muda rafiki akanitonya kuwa mchumba mjamzito. Aisee zilikuwa habari nzuri. Na kwakuwa yuko Moro mimi ikanibidi nichukue jukumu la kumuangalia shemeji. Shemeji alikuwa ananikwepa sana.

Kila tukipanga appointment hatokei na hapatikani. Bahati mbaya sikuwa nafahamu kwao kabisa ila nilikuwa na contacts zake.

Nikamuuliza rafiki kuwa shem yuko wiki ya ngapi? Majibu hana anajiuma uma hajui. Nikakwambia si amuulize? Akajibiwa wiki ya kumi.(Hapo hawajaonana).

Baada ya muda rafiki akaja Moro kwa siku mbili akaonana na mchumba wake na nilimsisitiza sana tena sana kuwa aone kadi ya clinic. HAKUFANYA HIVYO!! Na aliondoka kesho yake bila kuwa na uhakika wowote.

Mimi niliendelea kumtext shemeji na kuulizia anaendeleaje, na clinic na yuko wiki ya ngapi? Hakuwahi kunijibu.

Nikamwambia rafiki hii ngoma unapigwa changa(maana alishaanza kutuma hela). Hakuamini.

Anyways baada ya muda alikuja kugundua kuwa alikuwa anadanganywa na mchumba wake alikuwa muongo hakuwa na ujauzito na alikuwa na mambo 'mengi' mno. WAKAACHANA.

Kuwa makini sana kwenye hili. Ujauzito kutoka tena wiki ya 13 tena kwa mtu umpendae na akupenda si kitu rahisi cha kusahau tu. Peleleza. Kuna tatizo.
 
Haikuwa ya kwako hiyo kitu baba, kuwa mwangalifu sana na huyo dada
 
Sista nimefanya kila kizuri unachokijua mwanaume inabidi amfanyie mpenzi wake hadi nyumba inajengwa na kila kitu ni Jina lake. Kwa mwezi nilikua namtumia na bado namtumia si chini ya laki sita. Na tuko pamoja miaka 7 na nusu. What more can I do?
Bold: Mmmmmh! ndg una mioyo mingi aisee.
uchumba miaka 7 na nusu? Ongea nae kwanza ili ufanye maamuzi yanayotokana na maelezo mujarabu badala ya kuegemea hisia tu
 
 
Tigga mumba. Wakati anasema mambo ya klinik niliomba ushauri hapa jf na kama sikosei watu8 alinishauri aende na mtu au rafiki yangu. Nilimuomba mtoto wa kaka yangu aende nae na kweli walienda pamoja hila jamaa alibaki nje hivyo hakujua ya ndani yalivyoendelea na ilikua siku moja tu. Lakini naamini ulichosema mchumba wangu anaweza kabisa kua yuko hivyo ulivyo andika. Shukurani ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…