Nimeacha kuishabikia Arsenal

Chifu Ngongo umefanya jambo la maana sana katika maisha yako.

Karibu katika dunia ya raha, vicheko na tabasamu!

Kwa nini ujipe presha na wee clubs kama Arsenal?!?

Karibu leo tushangilie kuongoza ligi kwa tofauti ya pointu 15!

Cc: Wacha Wacha1 MwafrikaHalisi
 
Last edited by a moderator:
Mbona umechelewa sana? Mi nlishaihama mda mrefu,maisha yenyewe mafupi tena magumu kwelikweli halafu timu ikuongezee presha utafurahia wapi maisha na huna ugakika wa kwenda peponi? Hamia timu yenye kukupa raha..penda vizuri
 
Hongera sana Ngongo umefanya uamuzi wa maana karibu sana Old Trafold,karibu klub yenye mafanikio,karibu ukutana na kocha mwenye mafanikio,karibu upate rahaaaaaaaaaaaa.
 
karibu sana mkuu Ngongo, MAN U chama kubwa...Arsenal kweli presha za kumwaga si unawaona kina Wacha1, AW, BAK, Quesst, Viper n.k.

1st lady wa ManU@JF, Belinda!!!!!!
 
karibu sana mkuu Ngongo, MAN U chama kubwa...Arsenal kweli presha za kumwaga si unawaona kina Wacha1, AW, BAK, Quesst, Viper n.k.

1st lady wa ManU@JF, Belinda!!!!!!

Groly hunter au ni shabiki wa Manure ana ditch around chezea kuhama timu wewe
 
Mimi ni mshabiki wa Liverpool

kuishabikia Arsenal ni sawa tu na kuishabikia Totenham
wao wanatafuta 'the fourth place' kila mwaka
 
The Boss thread inahusu Ngongo kuhamia Manchester United wewe unaleta mambo ya Looserpool wapi na wapi.

Mimi ni mshabiki wa Liverpool

kuishabikia Arsenal ni sawa tu na kuishabikia Totenham
wao wanatafuta 'the fourth place' kila mwaka
 
Last edited by a moderator:
xo mbaya mgongo hujachelewa na nafac bado zipo kwa wahamiaji wapya karibuni MAN U
 
Hongera kwa uvumilivu hata hivyo umevumilia sana, umechelewa kuachana na ushabiki wa arsenal.
Baada ya kuacha kuishabikia arsenal, sina timu ninayoishabikia Uingereza. Bahati nzuri kwa spain nilikuwa naipenda Barca., kwa italy nilikuwa naipenda AC Milan ya kina Ruud Gullit, Marco Van Basten, na Frank Rijkaard. So far, ndio timu ninazoendelea kuzishabikia.
 

:biggrin1: karibu sana kwenye chama chetu hapa huwezi kupata pressure za maisha hata siku na sisi ni wakarimu welevu na wapenda amani kama ulivosema mwenyewe hapo juu....nimeshakutayarishia kadi yako ya uanachama na naomba uje na Viper Richard MwafrikaHalisi Wacha1 kashengo na wengineo ambao kucha wanakosa usingizi kwa sababu ya policies za kijinga arsene wenger na ivan gazidis wanazofanya....WELCOME TO OLD TRAFFORD....BEST CLUB IN THE WORLD AND MOST SUCCESSFULL IN ENGLAND
 
Last edited by a moderator:

hakuna kisichowezekana chini ya jua. Yani kuhama timu iwe ishu?
 

Mwandiko wako wenyewe unaonyesha hukuwahi kushabikia arsenal bwana. Kama kweli ulikuwa mshabiki wa Arsenal naomba ujibu hili. Ina maana miaka ijayo Manchester United wakija kuwa kama Liverpool au Nottingham Forrest utawakimbia? Mashabiki kama wewe hamfai hata siku moja. Mpira sio kama ndondi unapoweza kuhama toka bondia mmoja hadi mwingine. Kuna michezo mingi ya kufuatilia na kushabikia jaribu huo wa ndondi, draft, mdako, makida makida nk.
 
mm niko na chama langu liverpool na kamwe sintohama
Piga ua garagaza,hata nifungwe goli 10 nitabaki I will never walk alone
 
Hatua nzuri, lakini niko na swali kidogo.

Unapataje magonjwa ya moyo kwa timu za Ulaya, kilomita elfu kadhaa kutoka nyumbani kwako? Wakati mwingine wanawake huwa wanashangaa tunavyopigizana makelele na wengine hata kufikia kurushiana mangumi kwa mechi za Ulaya.

Athari za muda mrefu ni pamoja na kuporomoka kwa michezo yetu. Kama makocha, wachezaji, washabiki na wadau wote wako bize kujadili mustakabali wa timu za Ulaya ambazo ni kifurushi kingine cha ukoloni mamboleo, unadhani michezo yetu itapanda lini ili tulingane na hao munaowashobokea?

Hatuwezi kuamka japo kidogo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…