Nimeacha kuimba wimbo wa Taifa kwa hamasa......

Nimeacha kuimba wimbo wa Taifa kwa hamasa......

astig

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2017
Posts
204
Reaction score
248
Kwa jinsi siasa za nchi hii zinavyoendelea nimejikuta natafakari sana huu wimbo wetu wa taifa, nimetafakari maneno yaliyomo ndani yake.
Baada ya kufikiri kwa kina huku nikiwa nimeshaisoma sana namba katika hali zote. Kiukweli nimeacha kutaja yale maneno "wabariki viongozi wake" Hivi nawezaje kuyatamka huku nikikumbuka viongozi wenyewe ndio kama wajeuri hivi, tena "Makutubu" kama yule RC aliyepiga hela za rambirambi kule kaskazini, au yule Dc aliyerekodiwa alitoa rushwa, au huyu nanihii huyu (sijui vyeti) kwa hapa nyumbani. Mfano mwingine yule mhishimiwa aliyemlamba bakora mgombea mwenzake hadi akazimia kwenye kura za maoni. Yaaani hawa ndio wabarikiwe?
Kwanza naanzaje kuwaambia wabarikiwe wakati wanasema tutakiona cha moto?
Au kina Mu-7 aliyesema kila anachofanya ni kwa ajili yake na watoto wake, ama Yahya Jammeh (yule alieachia ngazi) na wengine wengi kwa nje.
Pia kuna yale maneno mwanzoni "Mungu ibariki Africa" Toka nimeimba ibariki Africa sijaona baraka zozote ktk bara hili zaidi ya laana za kutosha. Fikiria wale Wasouth Africa walioamua kuwafukuza watu weusi na kuwaacha weupe kwa kisingizio cha kuwachukulia ajira zao. Fikiria nchi kama Sierra leone, liberia na Ethiopia ambazo hazikuwahi kutawaliwa na wakoloni lakini mpaka leo ni nchi za umasikini wa kutupwa. Tumeimba sana Mungu ibariki lakini kila leo ni vita tu. Mara utasikia kuna waasi wameteka mji mkuu kule Sierra leone, then Congo sijui kuna M23, ghafla CAR vita vya wakristo na waislamu, mara coup de tat Mali, au utasikia jeshi linashikilia serikali Cote d Voire.Aaaaaaaaaghhh sasa ya kazi gani kuendelea kuimba hayo maneno wakati hakuna impact kwa Africa?

Afu why sisi ndio tunaipenda saana Afrika kuliko wengine? na mbona wakati "true son of Africa" alipouawa hakuna mwafrika yeyote alisimama kumtetea? Hivi kweli utake kumuua kiongozi wa nchi ya Ulaya then EU na wanachama wake wakuache?
Nashauri tupitie upya maneno ya wimbo wetu wa Taifa. Sio kesi kuu-edit
 
Mara ya mwisho niliimba kwa hamasa kipindi cha mgomo Mazengo tech
 
Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana
 
Tena kwa uzalendo mkubwa mbele ya mkuu wa mkoa hadi akapata kihoro
Huyo mkuu wa mkoa inaonyesha ni muoga sana.
Ila ilibidi aingiwe na kihoro maana si mchezo wimbo wa Taifa, wengine kwenye migomo huwa wanaimba ule wimbo wa "kama sio juhudi zako Nyerere"
 
Huyo mkuu wa mkoa inaonyesha ni muoga sana.
Ila ilibidi aingiwe na kihoro maana si mchezo wimbo wa Taifa, wengine kwenye migomo huwa wanaimba ule wimbo wa "kama sio juhudi zako Nyerere"
Nakumbuka alikuwa anaitwa Isdori Shirima,sijui yuko wapi now,ilibidi awe mpole ghafla maana wanafunzi wana hasira halafu wanaimba kwa uchungu mwingi mno.
 
Back
Top Bottom