Si lazima uishi nae kama huna mapenzi na mama yake.
Unachotakiwa kufanya awali ya yote, ni kuhakikisha unatoa huduma zote kwa mtoto, na kumwambia kuwa wewe ni baba yake. Hakikisha pia unamchukua nyumbani kwenu ili kuwajua jamaa zako pia.
Hilo nalifanya sana kaka, japo sifanyi kama vile mie nilifanyiwa..
Namtembelea mara chache sana na namwona anaathirika kisaikolojia, japo anasoma shule sasaa..!
Huwa natamani nimchukue lakini watu wananshauri nimwache kwa mamaye na nadhani wako sahihi..
Kuhusu kumtambulisha kwa jamaa na ndugu, ndio nimefanya ingawa ni kwa baadhi tu wale ambao naelewana nao vizuri.
Wapo ambao hawataki hata kusikia..! Inaniumiza sana as ni watu/ndugu wa karibu sana kwangu..
Hata pale niombapo msingi au msaada fulani husema hadi uachane na kumjali mtoto na huyo mwanamke..
Hapo huwa hatuendi sawa nao..
Muhimu ni kujua kuwa unachofanya ni jambo sahihi; kwako na kwa Mungu wako. Huwezi kuwaridhisha binaadamu wote daima dawamu
Wewe jitahidi uende kuonana nae zaidi ili mtoto ajue kuwa ana baba anaemjali. Mtoto wa miaka mitano si mdogo kuwa haelewi, mfahamishe kuwa wewe ni baba yake lakini huishi na mama yake lakini unampenda sana. Mara moja moja take him out just the two of you apate kukuzowea.
Muowe awe mke wako unasemaje?Umesha muharibia maisha yake, Hata kwa Mungu una makosa wewe ukimuacha Solelemba.
Kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa ndio kosa...sasa naona wewe unataka kulirudia...please muoe huyo dada ili mtunze huyo mtoto. Usiwe selfish kaka mfikirie na yeye...umemuharibia future yake...angefanya mangapi ya maendeleo hadi sasa bila ule ujauzito na mtoto aliyezaa...dhihiriisha uungwana wako kaka ... just marry her... mapenzi huja baadae... manake ht waliooana wanapendana baadhi yao ndo hawa tunakutana nao mahakamani wanadai au kutoa talaka zao...
honestly Swahilian nashindwa kukuelewa,are you feeling guilty kwa kuzaa kabla ya kuoa au una feel guilty kwa kuzaa na house girl? if it is the latter kwangu litakuwa jambo la kusikitisha sana maana ina maana ungezaa na airhostess au nesi basi usingefeel guilty? huo sasa utakuwa ni ni unyapapaa ambao haukubaliki.Kiila siku tunaimba humu mmu tujifunze kuwathamini watu si kwa sababu ya taaluma zao au pesa zao bali kwa sababu ya utu wao,umenipata Mkuu?Always remember housegirl ni mwanamke kama mwanamke mwingine yeyote na ana haki ya kupendwa na kuenziwa just like any woman!yees.! Thats what i do..
He also knows..
But guilty consiousness of wha i did past kills me slowly kaka!
Lini nitaliona jambo nilofanya ni la kupita/kawaida?
Hapo ndio pagumu kwangu...
But thanks@ Gaijin