Niliyoyapata baada ya kumaliza kuangalia series ya sky castle

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Hii series ndio nimetoka kuimalizia ilitengenezwa 2018 na ni moja kati ya series bora sana.

Imetengenezwa na JTBC huku ikipata wastani wa ratings 12.5% huku episode ya 20 ikiwa na ratings ya watazamaji 23%


Hivi ni vitu vitano usivyovijua kuhusu series hii :

1) Ilitakiwa iwe na Episodes 16 lakini ziliongezwa hadi 20.

2) Jina la kwanza lilikuwa ni "Princess Maker" lakini lilibadilishwa kuwa Sky Castle

3) Kiukweli ukweli hakuna sehemu inayoitwa Sky Castle nchini Korea. Series hii iliingiziwa hapo Seoul eneo moja hivi linaitwa Gyeong gi.
4) Jung Joon Ho ambaye aliigiza humu kama Kang Joon Sang pia aliigiza kwenye IRIS kama rafiki yake Kim Hyeo jun.


5) Wimbo uliotumika kama OST ya series hii "We all lie" ulidaiwa kuigwa kutoka kwenye wimbo wa "To The Grave" wa Bea Miller. JTBC walizima tuhuma hizo kwa kusema kuwa hakuna kitu kichoigwa,

SKY_Castle-GP.jpg
_6.jpg
Sky-Castle-Season-2-1280x720.jpg
AAAABbszqGL2q5YUB8bCTeHWIJviXy4uP8KOimmsltp4RNcd4Ezd5zMbTV4-J7pa2drYHpmdBypb8FpdpqVOj3RpT0mkTo...jpg
 
Ni seriea ya muda kidogo lakini kuanzia ubora wa picha, stori nzima na uhai wa waigizaji unaweza kusema imeigizwa jana yaani.

I must say Sky Castle ni series bora sana. In summary ni series inayoelezea mfumo mzima wa elimu ya South Korea ulivyo na namna ambavyo familia zenye uwezo zinatumia rasilimali nyingi kwenye kuhakikisha watoto wao wanaingia kwenye chuo cha Seoul National University.

Series hii imeshekheni visasi, uongo, mapenzi, drama na kikubwa kabisa ni namna ambavyo script yake iko relevant na maisha yaliyopo.

Kwenye Cable TV huko nchini South Korea series hii ni namba mbili kwenye orodha ya series zilizotazamwa sana kwenye nchi hiyo na kama umeiangalia sawa ila kama hujaiangalia hebu ingia kwenye kiss asian au Netflix ukajionee.

Sasa yafuatayo ni mambo machache niliyoyapata baada ya kukata series hii iliyotengenezwa na kituo cha JTBC.

1. WAKOREA WANATHAMINI SANA ELIMU.
Baada ya kuangalia series hii nikafahamu kwanini wakorea wako mbele yetu. Elimu Elimu Elimu. Wasomi nchini Korea wanaheshimika sana, tena hasa uwe umesoma kwenye Seoul National University, Korea University au Yonsei university.

Unaweza ukaona jinsi ambavyo Professor Cha aliyebobea kwenye sheria alivyokuwa anaheshimika au Kang Joon Sang alivyokuwa anaheshimika kuanzia kazini hadi nyumbani.

Na hii ndio sababu iliyomfanya Seo Jin mke wa Profesa Cha kumkazania mwanae asome au Jin Jin kumkazania mwanae ambae yuko primary asome kwa bidii ili aheshimike.

Tanzania mambo ni tofauti. Kuna watu wachache kwa sababu wana Vi IST wanapiga kampeni kuwa elimu ni kupoteza muda. Tena kuna wabunge kabisa wanasimama bungeni wanakandia mfumo wetu wa elimu. Its Sad. Tanzania leo hii mcheza forex kwa sababu tu anapata chochote kitu ni anaheshimika kuliko Profesa wa Udsm.

Nchi haiwezi kwenda huko. Lazima ifikie kipindi kila mtu apate heshima anayostahili. Hongera sana kwa Korea kusini kwa kutengeneza mfumo unaofanya vijana watamani kuwa maprofesa.

2. ELIMU SIO VITA.
Hiki ni kitu kingine. Muongozaji wa filamu anaonesha kuwa masomo hayatakiwi kuwa adhabu. Bali kusoma inabidi kiwe ni kitendo cha furaha tena kinachohusisha ushirikiano baina ya wanafunzi.

Tumuangalie Cha Min Hyuk au Professor Cha alicyokuwa anawafungia wanae mapacha Cha Seo Joon na Cha Ki Joon kwenye chumba chenye giza ili "waconcetrate". Na of course hawakuwa wanafurahi.

Au namna ambavyo binti Yeh Suh alikuwa mchoyo na notes zake lakini mwisho wa siku alikuwa anapata marks sawa na Hye Na

Sky castle imeeleza vizuri kabisa kuwa It doesnt matter unasoma kwenye ngazi ipi mwisho wa siku elimu ni ushirikiano. Share notes na wenzako, shiriki kwenye Group discussion na kutatua maswali kwa pamoja.

Yaani director Jo Hyun Tak amefanya kazi nzuri sana, kama unamjua mtu ambaye ni mchoyo kutoa notes zake au kushirikiana na wenzake mpe hii series inaweza kumsaidia.

3.KUAJIRIWA SIO KUBAYA.
Achana na motivational speakers ila huu ndio ukweli. Unaweza ukaajiriwa ukaishi vizuri kuliko hata huyo mtu anayejisifia kuwa amejiajiri.

Kwenye episode ya kwanza Suh Jin aliandaa bonge la party kwa ajili ya Young Jae, alimpa mwanae vitu vizuri in summary watu wa Sky Castle wengi walikuwa wameajiriwa kama madaktari na walikuwa wanaishi vizuri.

Hizi stori za siku hizi kuwa ajira hazipo au watu wajiajiri ni nzuri lakini haziko realistic kwa sababu ishu hapa ni kuishi vyema kama mtu umeridhika kuajiriwa kama Professor Cha au Professor Kang its fine. Usiruhusu mtu akupe presha ya kujiajiri huku maisha ni yako mwenyewe.

Kila mtu akifanya biashara nani atamtibu mwenzie? Akili za kuambiwa?

Uzi Tayari!
AAAABbszqGL2q5YUB8bCTeHWIJviXy4uP8KOimmsltp4RNcd4Ezd5zMbTV4-J7pa2drYHpmdBypb8FpdpqVOj3RpT0mkTo...jpg
20181224000716_0.jpg
sinopsis-drama-sky-castle-episode-7-ras-4cb0ef.jpg
Sky-Castle-Season-2-1280x720.jpg
 
Hongera kwa uchambuzi

Ila

Ulivyo taja korea tu hamu ya kuitafuta ikaisha na kuisha.

Kila la kjeri mtakao itafuta na kuitazama
 
Hiyo SKY ni kifupi cha vyuo vitatu Bora vya south Korea, na struggle za wazaz kuhakikisha watoto wanafanikiwa kuingia humo
 
Back
Top Bottom