Niliyoyaona Rwanda: Mazuri ya kuigwa na mabaya ya kuepuka

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
4,110
3,269
Wiki mbili zilizopita nilipata fursa ya kutembelea nchi jirani kwa mwaliko wa ndugu yangu anayekaa huko katika Province flani, wilaya flani(samahani kwa kutokuweka wazi). Kiujumla hali ya hewa ya ni nzuri kuna ubaridiubaridi. Kijiografia, karibia nchi nzima ni vilima(hills) na mabonde. Karibia ardhi yote inatumika kwa shughuli za binadamu. Sio rahisi kuona mapori. Hivyo ardhi ni finyu.

Nitaongelea niliyoyaona katika vipengele vifuatavyo:
1. Usafirishaji na miundombinu. Nilitumia njia ya barabara. Vyombo vya usafiri baina ya mikoa na mikoa au wilaya na wilaya ni coaster. Barabara zote zina lami. Kilichonifurahisha hapa ukifika tu kituoni ukakata tiketi inaonesha na muda wa kuondoka na ukifika tu mnaondoka.wapiga debe hakuna.

2. Biashara pamoja na ukusanyaji wa mapato. Maeneo ya kufanyia biashara yako kwenye mpangilio mzuri. Hakuna vibanda vya hovyo mijini, wala machinga. Complex zao zimejengwa vizuri kila wilaya. Kuna masoko pia ya vyama vya ushirika kila kata. Usafi unazingatiwa sana kwenye hayo maeneo ya biashara na bidhaa zao zinavutia sio kama bongo unaingia skononi unakuta ndizi zina matope.
Kwenye kukusanya mapato, hapa jamaa wako mbali sana aisee, kila biashara inayofanyika lazima ilipiwe kodi. Iwe saloon hata wakata tiketi za usafiri zinatolewa kweye mashine za EFD.

3. Suala la ulinzi na usalama. Hapa kidogo niliogopa maana muda wote mara polisi au wanajeshi wanapita pita tu. Ujambazi umeshasahulika kule. Ikifika saa 9 jioni, wanajeshi ndo wanaolinda taasisi zote za serikali na polisi wanaendelea na patrol. Hapa kuna cha kuiga Wanajeshi wetu pia wangekuwa wangepangiwa majukumu ya kusaidiana na polisi suala ujambazi lingedhibitiwa kwa kiwango kizuri. Nilishindwa kupiga hadi picha sababu ya hawa jamaa wanatanda sana barabarani huku wakiwa wamekoki mitutu yao. Suala la Rushwa na ufisadi pia limethibitiwa kwa 99%. Wafungwa pia wanatumika kufanya shughuli za kimaendeleo kama vile ujenzi na kilimo

4. Siasa, hapa raia wa kule hawajishughulishi sana na mambo ya siasa. Wanachojivunia sasa ni amani na maendeleo ya nchi yao. Japo bado watu hawaaminiani miongoni mwao kutokana na athari za mauaji ya kimbari. Hawashirikiani sana kwenye shughuli za kijamii kama vile harusi. Na sio rahisi kuchangiwa kama wewe ni mhusika mkuu.

5.Uchumi na Hali ya maisha ya kwa mtu mmoja mmoja. Ni kama huku kwetu, wapo matajiri na masikini pia. Vijana wengi wa kule wanapata fursa za ajira zenye malipo mazuri kwenye mashirika binafsi yanayofadhiliwa na wazungu. Walimu wa kule pia wana hali ngumu ya maisha kama huku Tanzania, mishaara midogo. Hapa ndo nilihitimisha kuwa viongozi wa waafrika suala la elimu sio kipaumbele sana .Pesa zao pia zina thamani kuliko za Tanzania. Laki moja ya Tz ni sawa na elfu 35 za kule.

6. Elimu, Afya na lugha. Wamejitahidi kuwa na mashule mengi na vyuo vikuu. Shule nyingi ni za mashirika ya dini na watu binafsi lakini zinatoa ufadhili kwa watu wasiokuwa na uwezo hadi vyuo vikuu. Hospitali pia zipo kwa kiwa kiwango kizuri na hapa kila mwananchi lazima awe na bima ya afya. Kama hana anaweza kataliwa kutibiwa. Kumbe hapa bongo watu wanabembelezwa sana, mtu anashindwa kulipia elfu 50 kwa mwaka ili kupata bima?. Kwenye lugha, Rwanda ni multilingual Society. Lugha kuu ni kinyarwanda, vilevile wanajua vizuri lugha za kiingereza na kifaransa. Sikupata shida sana kwenye mawasiliano maana hata bar, mabarmaid wanatema vizuri yai. Hapa Tanzania sijuitunapata ugumu gani wa kutumia kiingereza kufundishia toka shule ya awali na kiswahili kibaki kama somo? Ona sasa wenyewe wameongeza hadi kiswahili. Maprofesa wakatili hapo UDSM wanataka kufanya ukatatili kwa watu maskini eti kiswahili kitumike kufundishia hadi vyuoni wakati watoto wao wapo shule nzuri au nje ya nchi.

Kwa kuhitimisha, mambo mengi nimewasifia hasa suala la kutokuwepo ubabaishaji kwenye uendeshaji wa shughuli zao. Suala ubabaishji ndo limetufanya tufike hapa tulipo. Ona suala la vyeti feki, watu hawasomi kwa bidii wenzao wanasoma kwa tabu alafu baadae wanakosa kazi. Kila idara hapa huwezi kuwa promoted bila kuwa na mtu wa kukubeba. Nilitembelea pia kwenye makumbusho yao ya mauaji ya kimbari. Skeretoni zipo kama maonesho na makaburi ya pamoja.


Pongezi kwa Raisi wetu kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kuondoa ubabaishaji serikali, japo una shughuli pevu maana huku wilayani bado watu wanafanya wanavyotaka. Inawezekana hata na hili zoezi la vyeti wakakuhujumu, asilimia kubwa ya watu ambao hawakukamilisha uwasilishwaji wa vyeti vyao vina ukakasi.
 
Nani kakuambia bima ya afya bongo ni 50000? Ni 1,501,200 kwa private 50,600 kwa watoto na 76800 kwa waliojiunga kwenye vikundi tu pia kuna VIP na viongozi wa dini wana malipo yao bila kusahau waliojiriwa ambao muajiri wake amekubali kuwaunganisha kwenye bima husika ambao hukatwa 3% kila mwezi na muajiri nae analipa the same kila mwezi lkn kuna bima za wale wa vijijini 10,000 kwa mwaka.
 
Nani kakuambia bima ya afya bongo ni 50000? Ni 1,501,200 kwa private 50,600 kwa watoto na 76800 kwa waliojiunga kwenye vikundi tu pia kuna VIP na viongozi wa dini wana malipo yao bila kusahau waliojiriwa ambao muajiri wake amekubali kuwaunganisha kwenye bima husika ambao hukatwa 3% kila mwezi na muajiri nae analipa the same kila mwezi lkn kuna bima za wale wa vijijini 10,000 kwa mwaka.
Hapo ni kutokana na ubabaishaji tu. Ndo maana hata ukiwa na bima ya afya kwa sisi wafanyakazi ukienda hospital unaonekana kama ombaomba hivyo unapewa huduma ya hovyo au unaweza usipewe kabisa. Wabongo wao wanataka pesa mkononi kwanza. Tukiamua kila raia awe na bima inawzekana na hicho kiasi ni kikubwa sana hivyo tukishaipitisha hata gharama za mchango zinapungua.
 
Hata kama kuna maendeleo lakini kama raia hawana Uhuru wa kuongea ni kazi bure.madhaifu yanafichwa na wanajeshi na askari.nadhani Rwanda wananchi wangekuwa na Uhuru wa kuisema serikali na kuongea tungeyajua mabaya mengi zaidi ya hayo mazuri uliyoyaona.
 
Hapo ni kutokana na ubabaishaji tu. Ndo maana hata ukiwa na bima ya afya kwa sisi wafanyakazi ukienda hospital unaonekana kama ombaomba hivyo unapewa huduma ya hovyo au unaweza usipewe kabisa. Wabongo wao wanataka pesa mkononi kwanza. Tukiamua kila raia awe na bima inawzekana na hicho kiasi ni kikubwa sana hivyo tukishaipitisha hata gharama za mchango zinapungua.
Nakubaliana na wewe kuwa hii pesa ya mchango wa individual ni kubwa mno kwa mwananchi wa kawaida kumudu wanafaidika zaidi walioajiriwa lkn kuhusu huduma ya bima kudharauliwa ilikuwa siku za nyuma kwa sab NHIF walikuwa hawalipi kwa wakati lkn hivi sasa mahospital yanagombea kuingizwa kwenye list ya bima ya afya na kuna madirisha maalum ya bima ya afya huduma yake ni nzuri sana tena kama muhimbili ni nzuri kuliko hata wa cash halafu hakuna sababu ya manesi au madaktari kuwanyanyasa kwa sab wanalipwa mishahara yao whether wamhudie wa bima au wa cash.
 
Umesahau kutahiriwa

Kama wewe ni govi utakatwa

Naomba na hapa watu wa afya wapite kila nyumba kukagua na kukata
Asante mkuu kwa kuongezea. Ni mengi sana niliyayaona sio rahisi kuyasema yote. Nilisahau pia suala mpakani pale Rusumo, ukiwa unaingia Rwanda unakaguliwa kwenye mabegi, cha kustahajabisha ukiwa unaingia Tanzania ukitokea Rwanda haukaguliwi na polisi wa huku. Hapa kuna tatizo la usalama wetu.
 
Back
Top Bottom