Nilivyoshuhudia uchawi wa chuma ulete

Nilivyoshuhudia uchawi wa chuma ulete

Chumaulete haiwagi na pesa nyingi.. Ikizidi kbisa ni mwekundu
Mkuu nilikua nasikia hivyo Ila hii nimeishuhudia nadhani huyu alikua anatumia uchawi Kama ya wafanya biashara ya maduka makubwa au migahawa unakwenda Kununua vitu vya elfu kumi unashangaa umemaliza elfu hamsini Dunia Pana mkuu na marifa Kama bahari hayana mwisho.
 
Habari wakuu

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012 ndio naanza harakati za maisha nikaona kuishi na wazazi jau ngoja nikajipime maisha. Basi nikaanza harakati za kutafuta chumba nikafanikiwa kupata maeneo ya Buguruni kwa Madenge, katika hiyo nyumba, vyumba vyote vilikuwa na wapangaji ila kuna chumba kuna mpangaji alibakiza siku tatu ili ahame kwa maelezo ya yule dalali ni kuwa huyu mpangaji alishaambiwa ahame kama ikiwezekana baada ya siku tatu nije kukikagua nihamie. Nikaona sio ishu nikalipa kabisa kwakuwa nilipapenda tofauti na nyumba nyingine nilizooneshwa.

Siku ikafika nikawasiliana na mwenye nyumba akasema nije jioni huyu mpangaji atakuwa ameshaondoka, jioni mi nikatia timu nikakuta yule mpangaji ndio anaondoka basi nikaanza kuingiza vitu vyangu

Wakati naanza kupanga vitu vyangu ghafla nikamuona panya kwenye kenchi ameuma elfu kumi nikamtisha yule panya labda anaweza kuiachia zaidi yule panya akaniangalia akaanza kushuka kwenye chumba changu

Hiki chumba kuna kama choo ndani kwa ndani Ila hakitumiki kwa hiyo ni kama kastoo unaweza weka vitu vyako hako ka choo nikakuta tambaa limezingwa mfano wa ngata sikufatilia sana nikajua yule mpangaji amesahau nikimaliza kupanga vitu nitatoa na baadhi ya uchafu nikatupe

Basi yule panya akafika mpaka kwenye Ile ngata akaitema Ile elfu akapanda juu akatokomea wakati najiuliza kile ninachokiona yule panya akarudi kwa mtindo ule ule staili Ile Ile akaitema elfu kumi nyingine, kwakweli niliogopa ndio naanza maisha ya kupanga halafu siku ya kwanza nakutana na vituko

Basi nimemaliza kupanga vitu vyangu nikawa nimegemea kochi nikiendelea kutafakali ninayoyaona ghafla nikapitiwa na usingizi mzito. Kuja kuamka ilikuwa kama mida ya saa tano usiku nikamungalia yule panya sikumuona, nikainuka nikaenda kwenye kile kichumba hamadi! Nikakuta kwenye Ile ngata kuna elfu kumi kumi za kutosha kha mwanzo niliogopa baadae nikasema potelea mbali uchawi hauendi kwa mentali nikahesabu zilikua ni noti za shilingi laki moja na arobaini mh nikachukua nikazisunda kwenye begi chap nilikuwa na njaa hata njaa ikatoweka ghafla

Nikajilaza nikaja kushtuka na kelele za mlango wangu ukigongwa naangalia saa ni saa moja kasoro asubuhi ikabidi nishangae mm mgeni ni nani wa kuja kunisumbua asubuhi kama usafi si tullikubaliana na mwenye nyumba niwe nalipa pesa, kaenda kufungua namkuta ni mdada akasema yeye amehama Jana kwenye hiki chumba amesahau mzigo wake Tena amekasirika akiniuliza utanipa au nichukue mwenyewe nikamwabia siwezi kukupa kwakua sijui ni mzigo gani ukiweza ingia uchukue basi akaingia akafika mpaka kwenye Ile ngata akasimama kwa muda akachukua tambala lake akatoka bila kuaga Wala Asante, mh? Nikajua alaa kumbe huyu ni chuma ulete yule panya kazi yake nikuwaibia watu vyumbani chap nikaenda kwenye begi kuangalia pesa uph! alhamdulilah Ile laki na arobaini ipo

Hivyo ndio vituko vya uswahilini.
So alihama na kubeba kila kitu chake kasoro kileta pesa, au siyo
 
Ndio Ila namimi ilibaki kidogo niweke ngata yangu yamazabe Ila bimkubwa akaniambia aiwezi Fanya kazi kwakua yule dada tayari ana maagano na jini linalomuibia pesa
 
Hujachukua namba ya huyo dada aisee haya ndo mambo ya kushirikishana sio habari za kula kimashara
 
Ndio Ila namimi ilibaki kidogo niweke ngata yangu yamazabe Ila bimkubwa akaniambia aiwezi Fanya kazi kwakua yule dada tayari ana maagano na jini linalomuibia pesa
Embu tupe ushuhuda wa maisha yako hasa kiuchumi baada ya kuchukua zile hela kwenye ngata manake sio hela zako na pia sio hela za kawaida. Je ulipatwa na mushkeli wowote au upo vizuri tu tangu wakati ule?
 
Sikupata mushkeli Ila shida ya pesa za namna Ile hazinaga baraka
 
Mshana Jr embu rudi hapa tuondolee sintofahamu je hii ni chuma ulete au kuna maarifa mengine yamefanyika mkuu..
 
Back
Top Bottom