Nilivyopata kazi yangu ya kwanza

Nilivyopata kazi yangu ya kwanza

The Wolf

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
9,445
Reaction score
20,817
kuna dada yangu mmoja alikuwa anafanya kazi benki na pia alishafanya kwenye insurance companies, nilikuwa namuona namna anavyohangahika kutafuta wateja naakirudi home ni kulalamika tuu, saa nyingine tunabadilishana mawazo na kushauriana afanye nini, na kiukweli nilimsaidia sana kupata wateja(kipindi hicho mimi niko chuo mwaka wa pili), nilimrefer na hata kumpeleka kwa baba/mama/ndugu wa rafiki zangu kuna aliowapata na wengine waliomtosa. hii tabia ikanijengea ujuzi fulani katika masuala ya sales,hasa kutunga sera zangu kwa wateja na hata mameneja, ilinijengea confidence na ari ya kufanya kazi kabla hata sijamaliza chuo.

Baada ya kumaliza chuo, niliandika proposals tatu moja kwa meneja wa benki, nyingine kwa meneja wa kampuni ya ulinzi(kubwa) na nyingine kwenye kampuni ya bima. nilijitahidi sana kuwatafuta hawa mameneja hadi nikafanikiwa wa kwanza alikuwa wa kampuni ya ulinzi ambayo nilimuhakikishia kwamba nitamletea wateja wa kutosha na nikampa list ya uhakika ya watu (3)na makampuni(2) kama ninachotaka ni commision tuu sitaki ajira akasema hawezi kufanya hivyo sababu hiyo haiko katika sera ya kampuni yao labda waniajiri kabisa, tukaongea sana mwisho tukakubaliana kuhusu hilo la commision, nikaaanza kazi (mpaka leo hii nnaifanya akijitokeza mteja ninampeleka ninakula changu tena saa hivi malipo mazuri nimeshajitambua)

Hawa jamaa wa bima nao nilipata kwa mwendo wa commision(japo ni kidogo sana) kazi ikawa kwenye benki tuu(ndio nilipokuwa nataka kuajiriwa full time) nilienda kama benki tatu jamaa wananiona kama nafanya mambo ya kufikirika, benki ya nne nikaambiwa nipeleke wateja 10 kwanza kwa pamoja wanipe kazi, nikatimiza hilo maana hata ile kampuni ya ulinzi ilikuwa ni moja kati ya wateja wangu pamoja na walinzi 65 wa hiyo kampuni, ndo nikaanza rasmi kazi ya kuamka saa 11 alfajiri na kurudi saa 2 - 3 usiku. baada ya mwaka na nusu nikaacha kazi za benki baada ya kupata ajira inayoendana na taaluma yangu. Baada ya hapo nikafungua kampuni yangu mpaka hivi sasa nimeajiriwa, nimejiajiri na nimeajiri

Natumaini mtakuwa mmejifunza kitu hapa. Don't sit your lazzily at home, wake up and do something
 
Title ingekuwa "nilivopata demu wangu wa kwanza" mkuu 13 mega pixel hapa pangejaa likes! Bravoo braah, keep it up.
 
Last edited by a moderator:
"everybody is sitting on a diamond mine, just look around"
 
Powa bro lakn kumbka ulikuwa na msing kutoka kwa dada yako! Kwa njia hyo nam ntajarbu!
 
ni story yenye kutia moyo kwa wasaka maendeleo,baada ya kumsikiliza mengi jinsi kalamu zilivyomtoa unaweza msikiliza huyu kijana ukapata mzuka wa kutoa katik life hili la bongo kama una ndoto za kuwa na mafanikio makubwa.Big up mleta mada
 
Prove...kampuni gani? mwaka gani ulifanya nini na ikatokea nini? siyo mambo ya kufikirika au unatusimulia hadithi tu:A S wink:
 
now nnaweza kukuambia, securex kampuni ya ulinzi, Barclays bank, na reliance insurance timing sitakuambia, za siku mkuu?
 
Mkuu uliwezaje kutafuta wateja hasa.katika hiyo category ya kampuni za ulinzi? Bargaining namna ya kulipa haikuwa inakusumbua?
 
Advantage yangu ya kwanza ni connection na watoto wa kishua nilipokuwa nnasoma, hohe hahe tulikuwa wachache sana, pili nikaamua wanipe 10% ya malipo, tulishuka ikarange 5 - 8 kulingana na mteja, haikunisumbua kabisa
 
kuna dada yangu mmoja alikuwa anafanya kazi benki na pia alishafanya kwenye insurance companies, nilikuwa namuona namna anavyohangahika kutafuta wateja naakirudi home ni kulalamika tuu, saa nyingine tunabadilishana mawazo na kushauriana afanye nini, na kiukweli nilimsaidia sana kupata wateja(kipindi hicho mimi niko chuo mwaka wa pili), nilimrefer na hata kumpeleka kwa baba/mama/ndugu wa rafiki zangu kuna aliowapata na wengine waliomtosa. hii tabia ikanijengea ujuzi fulani katika masuala ya sales,hasa kutunga sera zangu kwa wateja na hata mameneja, ilinijengea confidence na ari ya kufanya kazi kabla hata sijamaliza chuo.

Baada ya kumaliza chuo, niliandika proposals tatu moja kwa meneja wa benki, nyingine kwa meneja wa kampuni ya ulinzi(kubwa) na nyingine kwenye kampuni ya bima. nilijitahidi sana kuwatafuta hawa mameneja hadi nikafanikiwa wa kwanza alikuwa wa kampuni ya ulinzi ambayo nilimuhakikishia kwamba nitamletea wateja wa kutosha na nikampa list ya uhakika ya watu (3)na makampuni(2) kama ninachotaka ni commision tuu sitaki ajira akasema hawezi kufanya hivyo sababu hiyo haiko katika sera ya kampuni yao labda waniajiri kabisa, tukaongea sana mwisho tukakubaliana kuhusu hilo la commision, nikaaanza kazi (mpaka leo hii nnaifanya akijitokeza mteja ninampeleka ninakula changu tena saa hivi malipo mazuri nimeshajitambua)

Hawa jamaa wa bima nao nilipata kwa mwendo wa commision(japo ni kidogo sana) kazi ikawa kwenye benki tuu(ndio nilipokuwa nataka kuajiriwa full time) nilienda kama benki tatu jamaa wananiona kama nafanya mambo ya kufikirika, benki ya nne nikaambiwa nipeleke wateja 10 kwanza kwa pamoja wanipe kazi, nikatimiza hilo maana hata ile kampuni ya ulinzi ilikuwa ni moja kati ya wateja wangu pamoja na walinzi 65 wa hiyo kampuni, ndo nikaanza rasmi kazi ya kuamka saa 11 alfajiri na kurudi saa 2 - 3 usiku. baada ya mwaka na nusu nikaacha kazi za benki baada ya kupata ajira inayoendana na taaluma yangu. Baada ya hapo nikafungua kampuni yangu mpaka hivi sasa nimeajiriwa, nimejiajiri na nimeajiri

Natumaini mtakuwa mmejifunza kitu hapa. Don't sit your lazzily at home, wake up and do something
Congratulations.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi za JK

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom