Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,981
- 45,902
Baada ya kuanza kutumbua majipu, baadhi ya wakosoaji kama kawaida yao walianza kurusha vijembe kuwa falsafa ya Magufuli haieleweki.
Kwa kuangalia mwenendo wa mambo nimeona Mh. Rais akiwa na mpango katika hatua tatu, nitaeleza.
Hatua ya kwanza: Kuondoa vikwazo Rasilimali watu; hii ndio iliyoanza kwa kuondoa wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wameshiriki katika kuliletea taifa hasara na kutufanya turudi nyuma kiuchumi, hii imetambulika kama kutumbua majipu.
Hatua ya pili; Kupambana na Changamoto; hatua hii itahusisha matumizi ya kila rasilimali katika kuona kwamba kila changamoto ambayo inaikabili jamii yetu inkabiliwa, kila aina ya changamoto ambayo ni kikwazo itafanyiwa utatuzi, hii itatupa picha halisi ya namna ya kupeleka maendeleo kwa wananchi, barabara sasa itakua wazi kwani changamoto zilizopo katika jamii zitakua neutralized na wale watu ambao ni tatizo watakua hawapo tena.
Hatua ya Tatu: Kupeleka maendeleo kwa wananchi; baada ya kuondoa vikwazo vyote na kufifisha chanagoto zote zilizokua zikituzuia kufikia malengo yetu, sasa inakuja hatua ya kupeleka maendeleo kwa wananchi, kama huduma bora za maji safi na salama, huduma za afya, elimu na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, kuongeza pato la taifa na shughuli nyinginezo za maendeleo.
Mipango yote hiyo itakamilika kama tukiweka jitihada pamoja kama Taifa na sio kuishia tu kukosoa kila kitu badala ya kutumia nguvu zetu na muda kujenga taifa.
Hivyo ndivyo nilivyoielewa falsafa ya Magufuli baada ya kuanza kwa kutumbua majipu.