Nilivyoingia gerezani kumtoa Mtanzania mwenzangu Afrika Kusini

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
4,134
5,243
Poleni na corona,

Wakuu maisha ni safari ndefu sana katika pilikapilika, mwaka 2000 nilienda Afrika Kusini kutafuta maisha...nilipelekwa na mama mmoja mkongomani aliyekuwa jirani yetu maeneo ya Tabata jijini dar es salaam.

Mama huyo alikuwa....
anajishughulisha na biashara za nguo huko SA na Tanzania,Kwa madiba alikuwa akiishi katika jiji LA Durban mji eneo LA free market.

Kwa wema wake aliamua kunichukua na kunisaidia kunifikisha SA niwe namsaidia kazi zake za kibiashara,kule yeye aliishi kama mkimbizi alikuwa na vibali vya ukimbizi kwa hiyo aliishi bila usumbufu,na kipindi hicho ilikuwa lazima uingie kwa viza.

Alinilipia kila kitu tukaondoka mpaka SA..kufika kule nikaanza kufanya kazi kwa kumsaidia ,alikuwa anauza nguo za mtumba kutoka msumbiji. katika soko LA free market...baada ya kuzoea kazi na mimi kwa miaka miwili nikapata mtaji,nikaanza kusima mwenyewe.

Katika ile kazi ya mitumba nilipata pesa,na maisha yakawa mazuri sana,nikapanga.... apartment katika mji Wa south beach,nikawa nasaidia nyumbani,nikanunia kiwanja nikajeng kibanda maeneo flani jijini Dar ,kwa hilo namshukuru sana mola kwa kusema.....ALHAMDULILLAH RABIL ALAMIIN.

Mwaka 2006 baada ya kuishi maisha poa SA ,nilirudi nyumbani kwa ajili ya kuoa lakini sikufanikiwa.....nilipoenda kumtembela anti wangu Tabora akaniambia kuna mjomba wangu amefungwa SA ...kwa kosa LA kuzushiwa kumbaka mteja wake,hakuniambia alikuwa akifanya biashara gani....licha ya kumuuliza sana lakini aligoma kunipa ukweli Wa kesi ya huyo mjomba ambae nilikuwa simfahamu.

Anti akaniambia kipindi narudi SA basi niondoke na dawa nimpelekee mke Wa mjomba, ambae simfahamu kabla ,anaeishi pale pale katika jiji LA Durban.Basi nikarudi SA kuendelea na mishe zangu huku nikiwa na ile dawa ya kienyeji iliyotoka Sumbawanga nilipofika nikamtafuta yule mke Wa mjomba nikampa ile dawa na maelekezo ya kufanya kisha nikaondoka zangu.

Kipindi nimerudi vibali vyangu vya kuishi kwa madiba vikawa vimeisha muda wake, yaani nime overstay......sasa ikabidi niende home affair kuweka mambo sawa....nilimkuta Dada mmoja baada ya kucheki passpoti yangu akaonesha mazingira ya kumpa rushwa ili anigongee,niendelee na mishe nikajikuta .....naduwaa maana usipotoa chochote unaenda jela kisha unakuwa deported....nilipigwa na butwaa, nikaja kupata ufahamu nimewekwa rumande ikapigwa simu nipelekwe jela mazima.

Nililala pale selo Siku moja...kesho yake nikapelekwa gerezani,huko gerezani nilikutana na wafungwa makatili sana ....asikwambie mtu...sema kule magereza yao ni bata sana..unakula mikate,mayai,maziwa,matunda basi kama ingekuwa bongo watu wangejaa segerea na ukonga.

Katika harakati za kutafuta selo nzuri ili ndio niwe naishi mle, Mara ghafla nakutana na MTU mule selo nikawa kama namuhisia kama ni yule anko....aliefungwa...nikamsogelea nikamsalimia Mara tatu...mpaka Mara ya NNE ndio akajibu nikamwambia anko nimetoka nyumbani nimepewa mzigo(dawa)nimempa mkeo ili utoke basi alishtuka sana!!!!!!

Akaniuliza wewe huku gerezani umefuata nini?
Nikamuelezea kesi yangu ya kuoverstay...akasema utaishi vizuri humu.Mimi nikiongozi usihofu hakuna nyau atakae kutisha mjomba.

Nilikaa na anko mle gerezani kwa amani na salama...baada ya mwezi mmoja kupita Mimi nilihamishiwa Jo'burg, nikapelekwa lindela tukarudishwa bongo na ndege....kufika airpoti migration.....familia ikanitolea elfu 50 shilingi nikaachiwa nikaenda nyumbani hiyo ilikuwa faini kama hauna unaenda jela kwa miaka hiyo.

Nilikaa bongo miaka miwili nikatafuta passpoti mpya nikachange jina, nikarudi bondeni baada ya kufika ,nilikutana na anko akiwa kisha achiwa ... tukaanza kupiga stori,ndio akaniambia ilikuwa nilazima Mimi kuingia gerezani ili yeye atoke gerezani LAsivyo asingetoka daah!

Nilisikitika sana...fikiria uteseke kwa kwenda gerezani kwa kesi ya mtu bila wewe kuridhia nilichoka sana aisee waswahili sio watu kabisa bora mabeberu.

Ile dawa niliyoleta ndio ilinipumbaza akili nikashindwa kumalizana na home affair mwisho wake nikaagukia jela,Ila niliamua kusamehe Mara sabini...mpaka sasa tuko pamoja na anko.
 
Nimesoma a to z,
Imekuwaje umeingia gerezani boss YAANI DIRECT KABISA MPAKA KWA JAMAA AMETULIA ZAKE MIAKA KADHAA HAPO NDANI UNAMUITA MJOMBA ANAITIKA?
Inawezekana vipi?
Siwezi kubisha sana, ila gereza za kwa madiba ninavyozifahamu, ni ngumu, japo inawezekana.
 
Kuna vitu kama hujaelezea vizuri mpaka baadhi watahisi umetunga japo mi nimrkuamini
 
Nimesoma a to z,
Imekuwaje umeingia gerezani boss YAANI DIRECT KABISA MPAKA KWA JAMAA AMETULIA ZAKE MIAKA KADHAA HAPO NDANI UNAMUITA MJOMBA ANAITIKA?
Inawezekana vipi?
Siwezi kubisha sana, ila gereza za kwa madiba ninavyozifahamu, ni ngumu, japo inawezekana.
Umesoma huku elewa,uliwahifungwa mwaka gani?
Mpaka ukazielewa.
 
Bro,umechanganya story
Unasema ulikuja TZ kuoa ukashindwa, je ungefanikiwa kuoa huyo mke ungempeleka SA wakati wewe huna uraia na visa yako ilikuwa imeisha?
Je huyo mjomba wako aliyekuwa amefungwa ulikuwa unafahamiana naye kabla? au ulimwona kwenye picha?
Kama hukuwahi kumfahamu ulivoingia selo ulijuaje kama ni yeye?
 
Bro,umechanganya story
Unasema ulikuja TZ kuoa ukashindwa, je ungefanikiwa kuoa huyo mke ungempeleka SA wakati wewe huna uraia na visa yako ilikuwa imeisha?
Je huyo mjomba wako aliyekuwa amefungwa ulikuwa unafahamiana naye kabla? au ulimwona kwenye picha?
Kama hukuwahi kumfahamu ulivoingia selo ulijuaje kama ni yeye?
Hujawahi ona mtanzania anaishi nje familia iko bongo basi tafiti.
Nilipewa taarifa zake na jinsi alivyo nimeamua kufupisha ili mengi yasiwe mambo...na ajabu iliyotokea nilipelekwa gerezani alilofungwa yeye.
 
Nimesoma a to z,
Imekuwaje umeingia gerezani boss YAANI DIRECT KABISA MPAKA KWA JAMAA AMETULIA ZAKE MIAKA KADHAA HAPO NDANI UNAMUITA MJOMBA ANAITIKA?
Inawezekana vipi?
Siwezi kubisha sana, ila gereza za kwa madiba ninavyozifahamu, ni ngumu, japo inawezekana.
Afrika kuna sayansi kubwa sana!
 
Back
Top Bottom