fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 5,609
- 7,169
Ni miaka mingi kama 15 iliyopita, mimi, dada zangu 2 na waume zao na kaka zangu 3 na wake zao,tulienda zanzibar kwa mwaliko wa rafiki wetu wa familia,ni mtu mkubwa serikalini hivyo siwezi kumtaja hapa.Kiongozi huyo alitualika chakula cha usiku kwenye hoteli moja hapo unguja.Kulikuwa na live band inapiga.Basi ikafika muda hiyo bendi ikakaribisha kama kuna mtu ana mziki wake,anataka apigiwe au yeye mwenyewe anataka kuimba,ajitokeze.
Kaka yangu akaniambia,ee jamaa we si sololist nenda kapige. Kama mnakumbuka nyuzi zangu za nyuma nikielezea kuwa mimi mziki naujua sana. Nikanyanyuka nijaenda mbele, nikaongea na band master kuhusu huo wimbo naotaka kuuimba na nitapiga solo,wakanisikiliza wakaanza kufatisha, mziki ukakubali. Badi baada ya dk 10 hivi tukawa tayari kuupiga wimbo huu:
Mimi nilienda,nikafika
Nikaambiwa lala nje,
Nukauliza kulikoni,
Nikajibiwa huna chako.
Nikaogopa nikarudiiiiiiiiiiiii.
Cha ajabu huu mziki ulinyanyua watu ukumbi mzima kucheza.Na nilikung'uka solo gitaa kwa ufundi mkubwa sana.wale wanamziki,wageni wote waliokuja walinishangilia sana.Cha ajabu kuna mzee mmoja alikuwa kakaa na mkewe na watoto wao 2 alilia hadharani na akaomba kipaza sauti akasema huo wimbo ni sawasawa na yale yaliyomkuta yeye.Sasa kaka na dafa zangu walicheka sana mpaka ukumbi mzima ulishaangaa,na kilichokuwa kinawachekesha ni kwamba huo wimbo ulikuwa unaimbwa na mwehu mmoja huko tulikozaliwa sisi.Ni kwamba wimbo waweza kuwa wa hovyohovyo tu lakini ukawekewa mziki na ukawa supa sanaaana