Nilivyo ibiwa kimaajabu

Ndefu sana au ni hadithi
 
Aisee
 
Chai
 
Stori ilikuwa nzuri hadi mambo ya ulozi yalipoanza nikaacha kusoma.
 
Naona watu wengi wanasema ni uongo. Si hayajawakuta. Yani kuna mambo humu duniani yanampata mtu, kama sio mtu wako wa Karibu unaemwamini ukisikia kwa mtu baki utasema ni uongo. Ila Hii dunia ina mengi jmn
Hayajawakuta bado ndio maana ila kwa tuliowahi kutokewa na haya mambo tunaelewa
 
Ulichokifanya kina nguvu sana,kokote pale na kwenye shida yoyote ile.
 

WACHA KUPAKAZIA , TOKA LINI JINA LA YESU KUONDOA JINI ??

mbona kuna watu kwa maelfu hii leo wanaitwa Yesu
 
Hypnosis
 
Hao jamaa wanatumia majini kuna waliofanya mchezo tuliwakamatia mombasa kwenye mil8 zimebaki tano
 
Hawa watu wanatumia dawa. Kuna dada nilikuwa nimepanga nae nyumba moja wakati nasoma chuo hapa Tanzania, yeye alikuwa anasomeshwa na wazungu wakiwa wanaishi ulaya. Tukiwa mwaka wa 3 chuo alitumiwaga pesa ya ada na kula kama milioni 6. Akaenda kuchukua KCB mlimani city, anapotoka tu akakutana na watu watatu mmoja mdada. Mmoja alipomsalimu tu kwa kushikana mikono, hakukumbuka kitu tena mpaka akili zilipomrudia akiwa geti la kuingia chuo kikuu UDSM pale mbele ya Savei. Hakujua hata amefikaje. Akiwa njiani na hao jamaa wanatembea tu kwa mguu kutoka mlimani city, mimi mwenyewe nilikutana nao Savei na nikamsemesha huyo mdada ambaye ndio ametapeliwa na akajibu salamu yangu kama hanifahamu, wakati tunaishi nyumba moja. Aliporudiwa na akili baada ya kutapeliwa akaja nyumbani analia ndio akanikuta mimi pale, na ndio akakumbuka kuwa nilikutana nae akiwa na matapeli na nilimsalimu.
 
Kuna Kijana mmoja alichezewa huo mchezo mlimani City mwaka sikumbuki.
Ila tukio lili repotiwa na chombo flan cha habari niliona dada akihojiwa.

Mwaka juzi Mama mkwe wangu..miaka miwili baada ya kustafuu akafanikiwa kumiliki Harier nyeusi.
Siku moja pale mafinga NMB akakutana na wagaigai wakamuita pembeni.
Kitendo cha Salam ya kushikana mikono.
Kilichofuata alianza kufuata maelekezo yao..
Sisi tulipata taarfa kwa watu wanaomjua kwamba Mama yenu kaokotwa forest huko hajitambui,nendeni hosptali flani mtamkuta.
Akatusimulia wahuni walimchukulia 7ml ila gari walimuachia.

Mm nilishawahi kukutana na jamaa wawili..nikiwa natokea Bank NMB.
Story ni ndefu kifupi tu,sikugusana nao mikono ila nilipewa kikaratasi nitafune (kosa kubwa)
Nilianza kusikia kusisimka na mawenge flani.
Walipo nitaka niwape simu na ela ..
Hapo hapo ndo nilistuka mazima..wakiwa wameniweka mtu kati...barabarani kabisa Nilikataa ,nikajitoa katikati yao nikavuka upande wa pili wa Barabara nikatembea mazima.
Nilinusurika kuibiwa na niliowaasimulia wengine waliamini wengine hawakuamini.

Utapeli kwa njia ya kishirikina Upo.
Ni halisi,kama hujawahi kutana nao huwezi kuelewa,na hapa duniani huwezi ukawa mwanafunzi wa kila somo mengine yatakupita watasoma wenzio,watakusimulia kazi ya kukubali au kukataa itategemeana upana wa akili yako katika kuchakata habari.
 
Noma poleni sana,
Sikuwai kutapeliwa hata siku moja mitego nilikua nabetua tu.
Ila kuna siku nililambwa roba ya mbao,jamaa wakaiba hela nyingi tu na dola za kutosha,
saa kali ya mjerumani breitling
Nilipewa zawadi tu.
Na moka zangu kali sana kipindi hiyo.
Nilikabwa kizembe mpaka leo najiuliza kwani sikuchukua taxi hadi maskani?
Hela ilikua debe mifukoni.
( za boss)
ILikua mapema alfajiri ndio nikala ngeta.
Na masumbwi kibao wakanisafisha tupa mtaroni nilizima.
Dah kile kisanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…