Niliuzika sana basi tuu!!

Haya matani yanaudhi sana wakati mwingine.. Ifike wakati yapigwe stop! Watu wanaweza gombana sababu ya utani!
 
utani ni kwa makabila ambayo ni wavivu kwasababu wana muda wa kutaniana
 
Maskinii.....polee!

Asante ila ndo hivyo tena nililoa haya matamaduni mengine yanatufanya wafrika tuonekane tunaishi kama sokwe moja wapo ni hili jambo la mamila na desturi ya kijinga
 
Waheshimiwa wadau wenza , nimefatililia michango yenu 1 baada ya nyingine, atlist Kongosho amejaribu.
Isichukuliwe kwmb wale waliotuzaa akili zao zilikua finyu laa ! Na sisi ndiyo tuko bora zaidi.
Haukuwekwa utani pasipo kusudio maalumu.
Navyofahamu shabaha ya utani mf.
Mzee Kaniki , ni Mz. Maarufu eneo analoishi, Mz mwenye pesa , na ni mwenye jina kubwa, ameoa na ana watoto.
Kupitia umaarufu wake , na mipesa yake , anatumia loophole hiyo kutembea na vibinti.
Vibinti ambavyo vingine ni vidogo kupita binti zake.
Inafika hata member wa familia yake wanatambua unajisi huo wa Baba yao.
Mz. Kaniki ameshatengeza mazingira ya kuogopwa sana na watu wa hom kwake,
na yote ni kuweka kinga , rejea tabia yake.
Na ndivyo itakavyokua hakuna atakaethubutu kumsema/kumkanya aache unajisi ndani ya watu wa nyumbani kwake. Hapo sasa watani ndiyo hufanya kazi/jukumu la kumfikishia ujumbe Mzee sampuli ya Kaniki. Iko mara mbili, familia ya mnajisi huweza ikawaomba watani private wafikishe msg kwa mlengwa , ama kama watani wamejua kwa vyanzo vyao, pia humfikishia msg Mzee muharibifu. Maneno kama mf.
- Una nini we Mzee cha maana we Mzee !
- Unajifanya una pesa ? Huna lolote maskini mkubwa.
- Alafu mchezo wako na vibinti vyetu tumeshaujua ! Subiri tuje tukukamate utaozea jela !
Ofcoz hilo la mwisho litamgusa na atajua tena bila mashaka kua uchafu wake ushatambulika.
Na hatimae atalazimika kuuacha unajisi wake.
Na hivi ndy ilikua purpose ya WATANI/UTANI.
 
utani ni kwa makabila ambayo ni wavivu kwasababu wana muda wa kutaniana

mkuu hata kukaa na maiti wiki mbili au tatu huku watu mnakesha kula na kunywa bia nayo ni uvivu tu kwa kuwa muda mwingi unatumika bure kwa kukaa na kunywa tu huku maiti ikizidi kuganda mortuary
 
Swali kwa Judgment na wengine je ni utaratibu gani ulitumika kutambua kabila x watani wake ni A,B na c? Au nani aliyepanga hiyo pattern ya kuwa mtani wa mnyamwezi ni msambaa?
 
ilikuwa njia ya kupunguza ukabila na uadui hasa kwa makabila yalopigana tanzania
nadhani idea ya mwalimu
japo siku hizi hauna mantiki tena
imebaki kusumbuana misibani na harusini

Asante mh Kongosho kwa ufafanuzi mzuri je ni vita gani iliyowapiganisha wanyamwezi na wasambaa hadi kupelekea leo kuwa watani leo hii?
 
Back
Top Bottom