Nilitembea naye kweli, akapata mimba... Lakini natatizwa na hili

Tukiwa tumebakiza siku au masaa kadhaa kuuaga mwaka 2022 nakuja mbele yenu na hiki kisa:

Kuna kabinti flani kalikuwa kanasoma chuo flani hapa Dom nilikuwaga na mahusiano nako miaka ya nyuma badae tukaja kuachana kama mnavyojua vidada vya chuo huwa vina mambo mengi.

Sasa mwanzoni mwa mwaka huu akaanza kurudisha mawasiliano na mimi tukawa tunachat mara moja moja akadai huwa ananimiss sana anatamani japo tupange siku tuonane tupeane utamu.

Nakumbuka ilikuwa tarehe 6 mwezi wa nne nilipata safari ya kwenda mkoa flani kucheck kama naweza kuwekeza biashara yangu ya majeneza huko, nikiwa huko nikawasiliana na huyu binti nikamjuza kwamba ntakuwepo hapo kwa siku kama tatu(kipindi hicho alikuwa anaishi mkoa huo baada ya kumaliza chuo)

Nilipomjuza kwamba niko maeneo hayo alifurahi sana akaomba kuja kuniona nikamkubalia hivyo akapanda basi kutoka eneo alipokuwa mpaka kufika mjini nilipofikia mimi ni umbali wa masaa matano hivi.

Ili kufupisha story alikuja tukapiga story kwa jinsi ambavyo tulikuwa na muda mrefu hatujaonana kila mmoja kammiss mwenzake tulijikuta room tunapiga show na tulilala mpaka kesho yake ambayo nakumbuka ilikuwa Karume day tarehe 7 April.

Kulipokucha ndo ananiambia eti tumesex siku mbaya ambapo anadai aliingia period tarehe 24 March hivyo kufikia hiyo tarehe tuliyofanya mapenzi tarehe 6 kuamkia tarehe 7 April ilikuwa siku ya 14 kwenye mzunguko wake hivyo anahofia kuwa kanasa mimba!

Nikamuuliza kwa nini hakusema kabla akasema eti kutokana na alivyokuwa kanimiss halafu alipofika tulikunywa kidogo hivyo anadai alijisahau amekuja kustuka asubuhi kwamba alikuwa tarehe mbaya!

Tuliagana nikaendelea na mishe zangu then nikarudi Dom tukawa tunawasiliana mara moja moja baada ya siku kadhaa akanambia amepima ana mimba na ana uhakika ni yangu!

Sasa mnamo jana tarehe 27 December huyu binti kanitaarifu kajifungua mtoto wa kike.

Nimekaa nikawaza kabla ya kuchukua maamuzi yoyote nifanye utafiti kwanza ili nisije kuwa napigwa na kitu kizito!
Najua humu kuna watu wenye uelewa tofauti hata wataalamu wa masuala ya uzazi pia wapo(japo wale wazee wa michambo pia wapo)

Naomba msaada wa kitaalamu kwa wenye uelewa wa haya mambo:

Inawezekana nisex na mwanamke siku ya 14 ya mzunguko wake ambao una siku 28 then aje kujifungua mtoto wa kike?

NB: Ikumbukwe kwamba alianza period tarehe 24 March na nikafanya naye mapenzi usiku wa tarehe 6 April na amejifungua tarehe 27 December mtoto wa kike!
Kaona maisha hayaeleweki baada ya chuo so katafuta pimbi wa kumwangushia mzigo na akakupata, inaezakana mimba ni yako kweli ila umepewa majukumu bila kutegemea so pambana baba... DNA yenyewe siku hizi wana discourage kupunguza watoto wa kukataliwa so ukienda na mood zako eti unahisi umeshikishwa wanakwambia mtoto ni wako so jipange baba
 
Mbwa dume leo mtoto huyo wakati unapata raha umekunjua unakojolea ndani hukujua kinachofuata ni nini au matokeo ya unachokifanya ni nini?

Haijarishi alikua kwenye siku zipi au amezaliwa mtoto mwenye jinsia ipi km kweli unathibitisha kwamba ulimmwagia ndani hio mimba inakuhusu, no way out lea mtoto
 
Yalinikuta mwakajana binti nilimla mara moja tu tarehe 23 mwezi wa kumi na moja.

After one month baada ya kuondoka yale maeneo binti akadai anamimba ilinipa wakati mgumu sana nikajua ananifanyia usanii, yalitokea mengi.. nikajisemea moyoni potelea pote nikaanza kulea mimba.

Tarehe 19 mwez wa nane mwaka huu kajifungua mtoto wa kiume, mtoto ni Aulu mtupu ningekataa ilikua aibu sana.

Nakushauri mtunze mwanao nakuwapenda siku zetu hazikawii kwisha fanya sehemu yako upite wee sio wakwanza.
Daa,baba bora
 
DNA ndio itatoa majibu sahihi, hizi zingine ramli chonganishi tu
Siku hizi hata ukienda kupima DNA hata kama mtoto si wako unambiwa ni wako maana unless kama mpo wababa wawili mnagombania mtoto ndo watawapa majibu sahihi kuhusu DNA
 
Tatizo linakuja kuwa baada ya kukinasa akawaza haraka wa kumwangushia jumba bovu na akiamini utakubali ni wewe so akarejesha mawasiliano na wewe na uzinifu wako ukaona mbunye imejileta yenyewe so ukumbushie enzi zenu 😆😆😆 bila kuwaza.
Kama siyo hivyo basi alipanga tangu mwanzo kuwa anataka kuzaa naye (labda amependezwa na mbegu yake?).

siyo rahisi kwa mwanamke kusahau siku zake kama anauelewa mzunguko wake
 
Aisee,wanaume bhana! Mi nakumbuka aliniuliza "mbona mtoto mweupe sana" wakati huo yeye ni mweupe wastani na ndugu zao weupe wastani...sasa nikajiuliza,INA maana kashindwa kutambua kuwa hata mtoto mweusi huzaliwa mweupe ...ngoz hubadilika taratibu....kwanza alisema toa mimba,nimepambania nizae tena mtoto mweupe sana.Hakika kuna muda wanawake tunapitia magumu kweli....

NB; kuna muda yai huchelewa kupevuka au kuwahi ivo mtoto ni wako.(wanaume jipunguzieni laana na kuongeza kizazi cha watoto waliokosa malez toka kwa baba,tunakufa jaman acheni kuzini bas kama hampendi majukumu Daa)

Nimejisikia vibaya juu ya huyo dada aisee

Ila wanaume
Hapo anatafuta excuse
 
Sio wa 3 ni wa 4 !

IMG_3065.jpg

Mimba inaanza kuhesabiwa period ya mwisho ambayo ni mwezi wa tatu

Mimba mpaka Leo ni week ya 39

Kujifungua ni kuanzia week ya 37


Manesi wa JF
 
Back
Top Bottom