Nilipomwambia nampenda alikataa katakata lakini kwanini ananiita "mpendwa"

Huenda unapendwa na wengine sio yeye
Nimetokea kumpenda huyu mtoto sana mwanzo alikuwa akiniita kaka, yaani kaka kwa nahisi hakupenda kunikata jina moja kwa moja.

Lakini siku zilivyoenda moyo ulimpenda sana sana, siku moja ikabidi nimwambie la moyoni akakataa na kwamba yeye bado hajakuwa tayari kuingia katika mambo haya ni mwanafunzi wa chuo ingawa kwetu ni kumoja. Alivyonambia hivyo wala sikumlazimisha nikatulia zangu.

Lakini cha kushangaza sasa akiniandikia sms kama kuniuliza hali huniita "mpendwa" ambapo jina hili limeanza mara baada ya kumueleza nampenda. sasa sijuw nishike wapi.

Naomba fatwa zenu wajuzi wa mambo haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimetokea kumpenda huyu mtoto sana mwanzo alikuwa akiniita kaka, yaani kaka kwa nahisi hakupenda kunikata jina moja kwa moja.

Lakini siku zilivyoenda moyo ulimpenda sana sana, siku moja ikabidi nimwambie la moyoni akakataa na kwamba yeye bado hajakuwa tayari kuingia katika mambo haya ni mwanafunzi wa chuo ingawa kwetu ni kumoja. Alivyonambia hivyo wala sikumlazimisha nikatulia zangu.

Lakini cha kushangaza sasa akiniandikia sms kama kuniuliza hali huniita "mpendwa" ambapo jina hili limeanza mara baada ya kumueleza nampenda. sasa sijui nishike wapi.

Naomba fatwa zenu wajuzi wa mambo haya.
Itakuwa ni mpendwa mtazamaji hiyo.Kaa chonjo
 
Hata Voda wananiita mpendwa. Mpendwa mteja tunakukimbusha kulipa deni lako la nipige tafu. Sio big deal wala nini.

Sent From Galaxy S9
 
Back
Top Bottom