Nilioyaona baada ya mechi ya Simba SC vs Kaizer Chiefs

yas-mic

JF-Expert Member
May 25, 2016
471
724
Kwanza kabisa kilichopo mezani ni kuwa Simba sc imetolewa kwenye Mashindano. hakuna njia nyingine ya ku justify simba's elimination in #CafCL lakini kuna mambo machache yametokea baada ya mechi ambapo binafsi nimeona kama ni kitu kipya sana kwenye mpira wetu.

1: Appreciation kutoka kwa mashabiki wa yanga:
Sijajua sehemu zingine za nchi lakini kwa ukanda ambao mimi nipo hili jambo kutoka kwa mashabiki wa yanga na watani wakubwa wa simba limenishangaza sana. Mashabiki wa yanga wengi wameonyesha kui appreciate simba kwa ilichokifanya na kutoa pongezi. hata mitandaoni kwenye page za watu maarufu kama akina shaffih dauda na millard ayo sijaona komenti zile za kubeza sana. kifupi wengi wameonyesha kuridhika na jitihada za vijana wa simba sc. kuna wakati natamani sana hili jambo liendelee la kuwa wamoja kwenye international tournament kama hizi japo najua haliwezekani

2: Great improvement in Tz football
Some years ago mafanikio makubwa ya timu zetu yalikua ni kufuzu round ya pili ya caf champions league. lakini mambo yamebadilika haraka sana mpaka kufikia kuiwaza nusu fainali na hata fainali. Haikua rahisi kuona shabiki wa soka wa Tz itafika wakati atasikitika eti kisa timu yake inashindwa kufuzu nusu fainali ya klabu bingwa afrika. Narudia tena, haya ni maendeleo makubwa sana katika soka la nchi yetu.

Tulizoea kuona mambo kama haya labda kwenye mashindano kama mapinduzi cup, tusker cup, kagame cup au Azam sports federation cup (Fa) lakini kwa sasa hadithi ni tofauti.

Hii ni dhahiri kuwa kwa sasa mentality ya kila shabiki wa soka wa TZ itaanzia ku focus timu zake kwenye group stage, quarter final na semi final. Hii ni inadhihirisha kuwa soka la Tz linakua.

Hongereni simba kwa kufungua njia, ni changamoto kwa timu za Yanga na Azam ambazo pasi na shaka mwezi wa 11 lazima zitakua kwenye ratiba za CAF kuweza kuenzi haya mambo. sio lazima sana simba afikie hatua hiyo tena lakini hata akifika yanga au azam bado itakua ni kielelezo cha kukua kwa mpira wa nchi na sio mpira wa simba sc pekee.

Let us push our football to the sky
Hongereni wana michezo
Hongereni simba sc supporters
Hongera kwa ceo
Hongera kwa mdhamini
Pongezi kwa Tff na Asante kwa serikali ya URT kwa kuweka mazingira rafiki ya kuchezeka kwa nchezo huu hapa nchini. Amani, upendo na mshikamano ndio unawezesha haya yote.
 
Mimi nilichojifunza, kumbe ndumba kuna wakati zinasadia kupata ushindi.
Hizo goli 3 tulizijua mapema kabla ya mchezo.
 
Mimi nilichojifunza, kumbe ndumba kuna wakati zinasadia kupata ushindi.
Hizo goli 3 tulizijua mapema kabla ya mchezo.
Ungewawekea wale vijana wa Coastal Union ya Tanga&African Sport na zikaleta majibu ningekuelewa nini unamaanisha.

Wale watoto ndio walioanza kushadidia ile kauli mbiu yenu ya NYUMA MWIKO ama kweli wakatia mwiko.

Achana na sisi wengine ambao tutakuta bangaloo tu kila mdudu hujikalia
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom