Hapo ni kukabana roba kwenda mbele, ukichukua mshahara leo, ujue si wako, ni wa watu kama 20 hivi. ukisikiliza sababu zao, unaweza kukimbia nchi.sio siri,kweli Tz ni ajabu la dunian ...
yaaan watu wanasimama majukwaani na kujitapa kwamambo meengi..
hamna kitu yaaani miaka 50 ya uhuru shule ya mjini kama hii... na sio hii tuu nadhan ni nyingi saana..
TUBADILIKE WA TZ KUANZIA MTOTO MWENYE UPEO MPAKA MZEE..
sasa tuzidi kushuhudia wimbi kubwa la vijana mtaani hawana kazi, elimu feki ndio maisha yatapendeza nadhani...
Habari JF,
Ni asubuhi na mapema niko ktk shule moja iliopo manispaa ya temeke, kigamboni Mjimwema, shule ya msingi Mjimwema, shule ilio anzishwa miaka takribani 40 iliopita na bahadhi ya viongozi wakubwa wamesoma hapo.
Naona wanafunzi wamekaa chini kwenye sakafu huku mwl akifundisha kwa bidii kweli!
Nikadhan labda ni mazoezi au ni masomo kw vitendo!
Macho yangu yaka zidi kuwa na hamu kubwa ya kutazama madarasa mengine nayo hivyo hivyo isipokuwa madarasa kama matatu tuu ndio kulikuwa na mchanganyiko wa waliokaa kweny madawat na chini!
Nilishangaa saana kuona hali hii kwenye shule iliopo mjini tena DSM pembezon mwa bahar ya Hindi!!
Ni ajabu lakin ni kweli, sasa je zile shule za kule sitimbi/vijijini ndio inakuaje sasa...?
Kw hali hii kwenye div 4 na 0 zitapungua, kwa nn watu wanaangalia shule za sekondari wana sahau msingi wa elimu uko wap?
Eti tume inachunguza matokeo mabaya..yaani una chunguza mwanafunzi aliengia kidato cha kwanza hajui kuandika jina lake!! Unatarajia atafaulu form4...
Tutarajie sinema na epsod za kutosha kwenye matokeo yajayo!!
Sikuweza kuweka picha wadau coz natumia ka nokia ka tochi!
Inategemeana una define vipi serikali. Hizo shule zipo chini ya serikali za mitaa (halmashauri) na ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha shule zake zinapata huduma zote zinazostahili. Sasa kama halmashauri hazijatekeleza wajibu wake, ilihali mkurugenzi wa halmashauri anateuliwa na Rais, kumbe alaumiwe nani? Kama si serikali tena kuanzia Rais aliyeteua Mkurugenzi asiyejua wajibu wake na bado hawezi kumwajibisha?Sasa ni kweli kabisa serikali ina upande wake wa lawama, hili la madawati kweli ni serikali nayo ndio ilete jamani? Kamati za shule zina kazi gani? bodi ya shule nayo? misitu yote hii, mi nasema watanzania tunahitaji kwanza ukombozi wa fikra zetu kabla ya ukombozi mwingine wowote ule, sisi ndio tunachakachua hela za ujenzi wa shule za kata, tunatoroka maofisini tunaenda kwenye dili zetu. hata kama serikali ni mbovu basi unahaki ya kuiwajibisha kwenye sanduku la kura lakini wewe je, umetimiza wajibu wako?
Nmesoma hapo darasa la kwanza mpk la nne
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Wewe ni mgeni hapa Yerusalem?