Nilimpenda lakini karudi na ujauzito usio wangu

Mimi ni mwanachuo katika chuo fulani hapa Tanzania. Kuna mwanachuo mwezangu girlfriend nilimpenda nikawa namsaidia fedha ndogondogo.

Wiki mbili zilizopita karudi kutoka field ana mimba sio yangu ila tuliahidiana kuoana lakini sasa yeye kaharibu, nifanyeje wakuu bado nampenda ingawa nimechukia. Nini madhara yake endapo nitaendelea nae age 24 Dem 22.

Hongera sana sana ila mwambie awe anatumia Condoms
 
Hongera kijana kwa kupata mtoto wakambo. Na wewe mletee mtoto wa kambo then hao watoto watawashauri wakikua.

Sikutegemea kama utauliza ushauri kwenye hilo
 
We muoe tu kwani mimba ndo nini
Upendo una nguvu kuliko mimba.
Ila badaye hushindwi kutumia hilo kosa kumchapia fimbo wewe
 
Kweli kua uyaone na sio maghorofa, ila nakupa hakikishi hata kwenye ndoa utaendelea kulea watoto wa wenzio sababu kashaona hiko kipaji unacho.
 
Unampendaje mtu ambaye ana mimba ya Mwanaume mwingine? huenda aliyempa mimba ana mpango wa kumuoa, jiongeze maisha mengine yaendelee.
 
Mimi ni mwanachuo katika chuo fulani hapa Tanzania. Kuna mwanachuo mwezangu girlfriend nilimpenda nikawa namsaidia fedha ndogondogo.

Wiki mbili zilizopita karudi kutoka field ana mimba sio yangu ila tuliahidiana kuoana lakini sasa yeye kaharibu, nifanyeje wakuu bado nampenda ingawa nimechukia. Nini madhara yake endapo nitaendelea nae age 24 Dem 22.

Unataka tukushauri ?
 
Yan sijui ndo malezi au nini ....nilipokuwa na umri kama wako sikua ndezi wa kiasi hiki duuu....hili mbona hata sio jambo la kuombea ushauri zaidi ya wewe "by now" kuwa ushaachana naye??
 
Mimi ni mwanachuo katika chuo fulani hapa Tanzania. Kuna mwanachuo mwezangu girlfriend nilimpenda nikawa namsaidia fedha ndogondogo.

Wiki mbili zilizopita karudi kutoka field ana mimba sio yangu ila tuliahidiana kuoana lakini sasa yeye kaharibu, nifanyeje wakuu bado nampenda ingawa nimechukia. Nini madhara yake endapo nitaendelea nae age 24 Dem 22.

Huyo tayari si mwaminifu hakufai
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom