Nilifikiri Moise Katumbi ni mnjanja kumbe wapi

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,793
Reaction score
5,053
Nilifikiri Moise Katumbi ni mjanja kumbe bado anatumia siasa zile za kupana sijui vitenge sijui mapipi sijui nini
Kuliko kujikita zaidi katika siasa za akili.

Afrika ukiwa chama pinzani hata uwe na wafuasi milioni moja na chama tawala kina wafuasi laki moja sio ajabu kuona chama tawala kinapita. Watu tunaendaga tu kukamilisha uchaguzi lakini matokeo wanapanga wao.

Ili kutoa chama tawala madaraka kwa mabavu ni kuwachongonisha na wananchi ili wafanye maandamo ya kutaka Rais ajiuzulu.

Hakuna jeshi lenye nguvu ndani ya nchi kama wananchi wenyewe wananchi wakisema imetosha ndugu yangu hata ulikuwa bado una miezi miwili madarakani unaondoka, kwa bahati mbaya wa Afrika hatujui hivyo ndio maana tunaongozwa na watu ambao hawafai kuwa hata viongozi wa kanisa.
 
Wewe acha matani bwashee, Congo DR wote ni wasanii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…