Nilidanganyaga wakaamini.... tupe nawewe ya kwako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilidanganyaga wakaamini.... tupe nawewe ya kwako

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Patrickn, Mar 22, 2012.

 1. Patrickn

  Patrickn JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 7,491
  Likes Received: 3,846
  Trophy Points: 280
  Wakati mdogo niliokotaga sh 5 nikaanza kushangilia... basi wenzangu wakaacha kucheza wakanizonga umeokota wapi na sisi tukaokote..huku wakinitolea mimacho... nikawaambia "nimeokota paleee...tena ziko nyingi.." (nikawaonesha jalalani)... wakaamini, wote wakakimbilia jalalani... kilichofuata ni kufukua jalala kuhamishia uchafu wote barabarani... mbaya zaidi namimi nikawaunga mkono... Haya tupe nawewe ya kwako
   
 2. kobonde

  kobonde Senior Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2010
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unanikumbusha mbali kipindi niko la pili, dada yangu alikuwa na mchezo wa kuiba coins ambazo zilitoka kwa wachota maji(wateja),kisha huzifukia chini na kuweka alama kisha ananiambia twende tukatafute hela na kweli tukienda tunazipata, lkn mara nyingi yeye ndie alikuwa anapata.Wakati mwingine ilinibidi nijidamke niwahi kuchimba Kabla yake lkn sikufanikiwa ikabidi nimsifie kwa mama kama mwenzangu anajua kutafuta pesa.Mama ndio akafanya uchunguzi na kugundua nini kilikuwa kinaendelea.
   
 3. Patrickn

  Patrickn JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 7,491
  Likes Received: 3,846
  Trophy Points: 280
  Hahahaaaaa... hiyo kali
   
 4. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka nikiwa darasa la pili walimu alitudaka na wenzangu wengine watano tunacheza muziki wa ndombolo ya solo, alichofanya ni kutusomba mpaka ofisi ya walimu akatupanga mstari mmoja na kutuamuru tucheze kama tulivyokuwa tunacheza darasani la sivyo tutarudi bila makalio, mzee tukaanza kusakata muziki sasa hivi ulikuwa unachezwa wimbo wa logaloga, basi acha walimu wavunjike mbavu ofisini, wimbo ulipoisha tukaachiwa bila kuchapwa bakora
   
 5. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nikiwa A level Tambaza,siku moja ijumaa narudi homu kinondoni argentina wikiendi kwa miguu nikakatiza kituo kidogo cha Polisi Hanannasif. Basi kumbe askari walikuwa wameweka uzio wao mtu akiruka wanamdaka wanamkamua mapene. Wakanidaka nikafungua mkata na kuvua viatu na kuzama lupango. Ilikuwa mara yangu ya kwanza,woga kibao.
  Dakika 2 mbele jamaa 1 na mkewe wakadakwa wakalipisha na kuondoka. Akili ikaja,nikamwita afande nikamwambia,"alo kwenye mkoba wangu kuna notebook,naiomba nikupe namba umpigie mdingi aje anitoe!"
  Afande: Babako anaitwa nani ?
  Mimi : ACP Kipingu,Mkuu wa Gereza Ukonga.
  Afande: Atufanyi kazi hiyo,wewe unalala apa adi jumatatu.
  (Akarudi kaunta).
  Dakika 5 mbele nikamsikia akimwambia mwenzake,"Pot lifungulie litoto la Afande likapate lanchi."
  Mazee nilipotoka, viatu na mkanda nilienda kuvalia mita 200 mbele. Afu nduki home. Sikuwahi kukatiza tena pale.
  Ajabu sikuwa na notebook wala namba yoyote ya simu,niliamua kuwatisha wale maafande waniachie. Mdingi wangu hakuwa askari ila pale Ukonga nilikuwa na anko angu mwalimu wa primary school.
   
 6. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Umenkumbusha dada yangu,enz izo ana boyfriend,biznesman wa Mbagala,wakati ye da J, anasoma st antony,bas anachelewa kutoka shule,kumbe anakuw kw shem..siku moja vkamnogea akaamua akache buku kabisa ahamie kwa mshkaji,home tafuuuta hadi polis,lakini wapi,..kukaa week 2,akarudi eti kajipaka unga katibua nywele,anaongea kama ndo kwanza anaanza kutamka maneno..et "nlikuwa msukule,wakataka kunikata ulimi,nkakimbia,et nlikuw porin rang3",enzi izo hakujajengwa.Teh cku shogake aliejua akatoboa siri mbele yangu,..bila kujua..namimi bila hiyana nkamtolea copy maza! Da J akapewa kibano ova cha kibaka wa cmu,akasema vyote!akahamishwa kabisa akapelekwa bording school!
  Alinimind mbaya,ad anamaliza shule hatuongei..adi cku ya graduation yake,teh but im glad she is mybestfriend now,kakua kaacha,yupo na mchumbake yuleyule,married with2kids.
   
 7. Rosweeter

  Rosweeter JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 1,136
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Ha ha haaaaaaaaaaaaaa... I like this
   
 8. sister

  sister JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,028
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  hahahhahahah, wakati niko la tano kuna dogo alinitukana darasani basi na mimi nkaenda kwa mwalimu kumsemelea mwalimu akaniambia kamuite alivyokuja mwalimu akaniuliza eeh amekutukanaje nikamtajia lile tusi basi mwalimu akasema nendeni mana na wewe umeshamtukana kwa hiyo umeshamrudishia.
   
 9. E

  Erasto toga Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yupo mpenz wang enz hzo za kulala mchana! Maza akawa anamaind kiseng af wenyw hawatak kulala so wakawa wanacheza kitandan! Siku moja maza akawafuma wanacheza af wakampotezea kidizain flan hv et wamelala! Maza si kauliza aliye lala kwel anyooshe mkono juu kama hujalala fimbo! Lol! Shemej yenu hajanyoosha mkon! Alifinywaje xaxa!
   
Loading...