maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,341
- 15,829
Wakati mdogo niliokotaga sh 5 nikaanza kushangilia... basi wenzangu wakaacha kucheza wakanizonga umeokota wapi na sisi tukaokote..huku wakinitolea mimacho... nikawaambia "nimeokota paleee...tena ziko nyingi.." (nikawaonesha jalalani)... wakaamini, wote wakakimbilia jalalani... kilichofuata ni kufukua jalala kuhamishia uchafu wote barabarani... mbaya zaidi namimi nikawaunga mkono... Haya tupe nawewe ya kwako