eneo hili linaitwa MAGHARINI. liko jimbo la muleba kusini kwa bi. anna tibaijuka. mwaka jana nilikuwa eneo hili kikazi. nikavutiwa sana. hadi nikafanya mahojiano na mdau mwenye kibanda cha soda juu tukio hili la kustajabisha. akaeleza kuwa alikuwepo mdau kijana mwenye magonjwa ya akili aliyeishi hapo muda mrefu, akawa anakusanya chupa za plastiki, ndoo, magalon na kuyafunga kwa ustadi kwa kutumia kamba kisha kuyaning'iniza (pichani). mwaka juzi walikuja wazungu wakastaajabu kazi ile na walipododosa wakahitaji kukutana na huyo kijana. wwnyeji wanasema waliondoka naye hadi sasa haijulikani yuko wapi, alipona, aliongezewa maarifa (utundu). *chanzo: simulizi fupi kwa wenyeji.