S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Nilichojifunza MTVmamaAward2016 jana.
Mosi, tujipongeze Watanzania kwa kuanza kujipenyeza kwa wingi katika mashindano makubwa zaidi Kimziki Duniani chini ya MTV. Japo hatukuchukua tunzo yoyote, Mimi nasema ni hatua na tusife moyo kabisa. Kuwa na wasanii watano kwenye mashindano makubwa ni hatua kubwa mno. Jana tulimuona Diamond Platnum, Ally Kiba,Navikenzo,Yamoto Band, na Vanesa Mdee. Hii ni hatua kubwa sana kwa wasanii wetu na Hongeeni sana sana.
Pili, kushindana ni mkakati mkubwa, Wanigeria wamechukua tunzo nyingi zaidi, ni kweli walianza mapema na kugundua FURSA hii ya mziki kimataifa na sisi ndiyo tumeanza kujua FURSA hii. Hapo nyuma kuna wasanii wetu walijaribu kujipenyeza lakini niseme sijui walikosa watu wa kuwapenyeza zaidi ikafikia hatua wakakata tamaa. Nakupongeza AY kwani wewe umekuwa mfano mkubwa zaidi kuwaonyesha Wanamziki wa Tanzania umuhimu wa kufanya mziki wa Kimataifa.
Tatu, kama nilivyosema, inahitaji mikakati mikubwa zaidi kushinda, kwanza ili ushinde lazima uchaguliwe na watu wengi kwenye kundi ambalo umeteuliwa kushindana na wenzako. Wanageria wao wanajua na wala hawakuwa na U-Team Diamond na Ally Kiba. Wanaigeria wao waliwachagua wakina Wizkid,Techno,Yemi Alade, na Patoraking kwa wingi sana. Wanajua sana umuhimu wake wa kuwa brand wasanii wao. Ni kweli, wanatuzidi kimziki lakini wengi wetu sisi ni kushabikia tu badala ya kupiga kura. Na hata tukipiga tuna onyesha U team badala ya kuchagua wote bila kujali uteam wowote. Hili ni somo kubwa tunatakiwa tujifunze huko mbele.
Nne, watu wengi kutojua kinachoendelea Duniani. Wengi tumekalia kujua sijui Wema kafanya nini mitaani badala ya kuangalia wasanii wetu wanafanya nini Duniani ili tuweze kuwaBrand. Wasanii wetu wakijulikana Duniani ni ajira kubwa zaidi kwa vijana wetu na wataonyesha njia kwa kizazi kidogo.
Tano, kwa wizara husika ya Michezo na Sanaa, pia tukubaliane tu kwamba bado tuko nyuma, wakati mwingine inabidi tu kuwakumbusha Watanzania kitu gani kinaendekea Duniani kwa Michezo yote na Sanaa zote hii itasaidia sana kuwafanya wasanii wetu kuchaguliwa na kuchukua tunzo. Nchi zingine kama Nigeria wananchi wake wanajua kwani wanafatilia na ndo nchi ambayo inayoongoza kwa wananchi wake kufanya kazi nchi za nje. Ni vyema tukawajulisha yanayoendelea.
Kwa vyombo vyetu vya habari, navyo vinawajibika kuwakumbusha Watanzania mambo yanayoendelea Duniani. Ni ufahari mkubwa kuchukua tunzo za Kimataifa. Vyombo vyetu vya habari ni somo kwetu.
Mwisho, kuna wasanii wakubwa kama wakina LadyJaydee, ni sisi hapahapa tumewadogosha, sijui kwa sababu wanadai haki zao za msingi hata sielewi. Leo msanii Yemi Alade anachukua tunzo, nina uhakika leo MTVmamaAward2016 jana tungemuona LadyJaydee, lakini tumekubali kumdogosha kwa sababu ambazo huwa sizielewi mpaka sasa.
Simon Ngusa Jilala
23/10/2016