Wana-JF,
Baada ya kutazama mkutano wa Chadema uliofanyika Jangwani (26.05.2012) na wa CCM leo tarehe 09.05.2012,nimejifunza kwamba CCM imechokwa na wananchi walio wengi, hivyo CCM imebaki ikitumia mbinu nyingi sana ili kuwadhiirishia umma kwamba bado inapendwa na wananchi lkn si kweli. Nasema hivyo kwasababu zifuatazo,
1. Umati wa watu waliohudhuria leo Jangwani kwenye mkutano wa CCM bado haulingani na wa CHADEMA. Ukiangalia kwa makini utaelewa hiki ninachokisema, kwani leo watu wamekalia viti na kwa kawaida viti vinachukua nafasi kubwa tofauti na wa CHADEMA ambapo hakukuwa na viti na watu wengi walisimama. Katika hali ya kawaida, kiti kimoja kinaweza kuchukua nafasi ya watu 3-4 waliosimama.
2. CCM wametumia motives na incentives nyingi sana kuwahamasisha watu kuhudhuria kwenye mkutano wa leo. Motive walizotumia CCM ni kama usafiri, pesa na vitisho kwa walio wanachama wa CCM kimwili na si kiroho kuhudhuria mkutano wa leo. Nasema hivyo kwasababu pale Jangwani leo kuna watu ambao wamehudhuria tu kwasababu hizo nilizotaja hapo juu lkn si kwa hiari yao. Hili ni tofauti kabisa na CHADEMA ambao hakukuwa na motive yoyote ile tofauti na watu hao hao kutakiwa kuichangia CHADEMA kwa kile kidogo walichokuwa nacho. Ukiangalia hili utagundua kwamba ni kweli kwamba siyo wote walioko Jangwani leo wanaipenda CCM kutoka moyoni, HAPANA, nasema hapana tena kwa herufi kubwa kwasababu CCM wana Dola na CHADEMA hawana dola, hivyo CHADEMA haina nafasi ya kumtisha mtu yeyote tofauti na CCM yenye DOLA:
Hivyo, napenda kuhitimisha kwamba CCM wana kazi kubwa sana, kwani wengi walioko pale Jangwani leo wapo kimwili kwasababu ya PESA, USAFIRI, na VITISHO lkn KIROHO wako CHADEMA. Na kwa msingi huo naamini kwamba CCM wana kazi ya ziada ya kufanya ili kurejesha imani ya watanzania walio wengi. Nasema CCM wana kazi ya zaida ya kufanya tofauti na ilivyo sasa ambapo CCM imekuwa ikidandia KILA KITU TOKA CHADEMA. Hili liko wazi kama ifuatavyo,
1.CHADEMA walikuwa wa kwanza kuzindua M4C na sasa CCM nao wameiga.
2. CHADEMA walipofanya mkutano wao Jangwani mwezi jana, ghafla mapema mwezi huu CCM nao wanafanya mkutano Jangwani.
3.Chadema walipohamia kusini, Mawaziri wa CCM wamekimbia ofisi zao na kurejea kufukia mashimo huko mikoa ya kusini.
4. N.K
NB1: Swali la kujiuliza hapa ni JE CCM SASA WAMEFILISIKA KIASI KWAMBA WANASUBIRI KINACHOFANYWA NA CHADEMA ILI WAIGE? Je CCM AMBACHO KIKO MADARAKINI TOKA 1977 mpaka leo bado haina ubunifu wowote kiasi kwamba inakaa mlango wa nyuma ikisubiri CHADEMA wabuni kitu,ndipo CCM ijitokeze na kuiga? HII NI AIBU KUBWA SANA KWA CCM.
Je kwa UIGIZAJI huu unaofanywa na CCM, je kuna haja ya kuwalaumu hata mawaziri ambao hawana uwezo wala ubunifu wowote, kwani wao ni zao la CCM ambalo sasa kila siku inalala na kuomba CHADEMA wabuni kitu kingine ili wao nao waige.
NB2: Baada ya CCM kukosa ubunifu na kubaki kusubiri CHADEMA wabuni ili waige, sasa nimeelewa ni kwanini Viongozi wengi sana wa CCM wanajipa PHD ambazo hawajazisomea na hakuna anayewakemea. Ukiangalia CV zao hata qualifications za kuwawezesha kuitwa Dr., hawana lkn wanajiita Dr., refer Waziri wa Fedha wa sasa, Mwanjelwa yule wa Mbeya viti maalum, n.k, n.k. Huu pia ni uigizaji ambao umebuniwa na CCM lkn wenyewe wameuiga kutoka nje ya nchi bila kujua kwamba je ni kwa VIGEZO GANI mtu anastahili kuitwa Dr.?
Nawasilisha.
TELO.