Nilichogundua kwa siku ya leo

Nilichogundua kwa siku ya leo

LIGEDENGE 1

Senior Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
184
Reaction score
29
Hakuna hata malori wala mabasi ya mkoa yanayoingia wala kutoka dar. Morogoro road nyeupeee...zipo daladala na gari ndogo tu.
 
Kuna siku Dar es salaam itabaki kama kisiwa. Hebu fikiria kama Morogoro road, Bagamoyo road na Mbagala zikifungwa tutatokea wapi?
 
Sababu ya mafuriko Ruvu mkuu. Mvua za mwaka huu zinatisha aisee
 
Hakuna hata malori wala mabasi ya mkoa yanayoingia wala kutoka dar. Morogoro road nyeupeee...zipo daladala na gari ndogo tu.

Mkuu kwa leo Mbezi Mwisho hadi Posta ukiwa na private car unatumia dakika 30 hadi 40 wakati siku nyingine huwa ni dakika 90 hivi.

Ni kweli sababu ni hiyo ya kutokuwepo kwa malori yanayoingia jijini, kwa kawaida kuanzia alfajiri ya saa 11 msururu wa malori huwa unaanza kujilimbikiza pale Kimara Mwisho na kadiri muda unavyojongea foleni nayo hukua taratibu na baadaye huamia Ubungo.
 
hii hali iendelee waonaje...? ndio maana huku kwetu njia panda segerea haina magari yatokeayo huko...
 
Madhara ya hii mvua yanatisha sana...
 
Hakuna hata malori wala mabasi ya mkoa yanayoingia wala kutoka dar. Morogoro road nyeupeee...zipo daladala na gari ndogo tu.

Natamani nchi nzima ijae mafuriko huenda tukatia akili!
 
kuna jamaa humu kwenye daladala,kasema alshabaab wakifanyizia dar kwa leo hatoki mtu. airport nako ndege haziruki,lindi hakuendeki,rudi chalinze nako fyongo. bagmoyo ndio usiseme.
 
Mkuu kwa leo Mbezi Mwisho hadi Posta ukiwa na private car unatumia dakika 30 hadi 40 wakati siku nyingine huwa ni dakika 90 hivi.

Ni kweli sababu ni hiyo ya kutokuwepo kwa malori yanayoingia jijini, kwa kawaida kuanzia alfajiri ya saa 11 msururu wa malori huwa unaanza kujilimbikiza pale Kimara Mwisho na kadiri muda unavyojongea foleni nayo hukua taratibu na baadaye huamia Ubungo.

sababu tumepata,watatue tatzo sasa
 
Kuna siku Dar es salaam itabaki kama kisiwa. Hebu fikiria kama Morogoro road, Bagamoyo road na Mbagala zikifungwa tutatokea wapi?

Kabisa sanjo. Miundombinu ya Dar imechoka
 
Usijiombee mabaya,kwani hata wewe utakuwa mhanga pia

Unadhani mimi ni kama wale ambao wanakwenda vitani lakini hawataki kwenda mstari wa mbele?

Hapana

Ninapotaka haya ninamaana hata mimi yanifike pia maana wapu.uzi ni wengi sana na kufikiri kwao ni dhambi

Yatukute na kubaki hatuna kitu kabisa huenda tutajua thamani ya kufikiri!
 
Ikiendelea kidogo subiri bei ya chakula ipande hapa mjini,
 
Unadhani mimi ni kama wale ambao wanakwenda vitani lakini hawataki kwenda mstari wa mbele?

Hapana

Ninapotaka haya ninamaana hata mimi yanifike pia maana wapu.uzi ni wengi sana na kufikiri kwao ni dhambi

Yatukute na kubaki hatuna kitu kabisa huenda tutajua thamani ya kufikiri!

Unafikiri hiyo ndio itakuwa solution?
 
hii hali iendelee waonaje...? ndio maana huku kwetu njia panda segerea haina magari yatokeayo huko...

Hahahah!!!

Mkuu uwepo wa mafuriko si suluhisho la foleni barabarani, mwarubaini wa foleni ni kuongeza tu idadi ya barabara na kuboresha zilizopo...pia kupunguza utegemezi wa eneo moja kuwa ndio kitovu cha shughuli za kiofisi au kibiashara.
 
Back
Top Bottom