Niliachwa kisa elfu sitini


inaendelea:alidondondosha(hata hivyo sikumwamini sana maana ana tabia ya kuuza simu)akakaa bila mawasiliano nami kwa siku tatu,siku ya nne akanisms kwanza halafu akanipigia na kuniambia,mm nikasema nina simu hamna haja ya kununua nyingine,basi akakubali nikampa ila sikujua mwenzangu anataka hela. Maisha yakaendelea ila mwenzangu akawa yuko busy na anafanya timing ule muda anaojua kwamba nitamtafuta yaani kama nampigia saa nne yy ataanza kuongea saa mbili,tukagombana weee,marafiki zangu wakanishauri kwamba upendo wangu utaniponza maana huyo kaka hana mapenzi ni mtaka vitu, Basi kutokana na namba yake kuwa busy na maumivu kila siku tukapanga kuonana ila lengo ni kumnyang'anya simu na nilfanya hivyo kwa hasira kweli na kuiuza kwa bei ya hasara yaani hakuamini,baada ya siku moja akaniita huku ana simu ambayo haifungi kwenye betri na alirudisha mawasiliano kwa nguvu kuliko mwanzo ila moyoni niliapa hapati hata mia yangu.Nikamwambia jinsi anavyoniumiza kwa kuwa anajua nampenda naomba tuwe marafiki wa kawaida tu,baada ya wiki akarudi kwa kasi na kuomba tuonane na kuomba msamaha,akaniambia kapata elfu sabini anaomba nimsaidie elfu sitini anunue nokia asha,nikamwambia nakupenda sana ila kwa sasa siwezi kukusaidia hata mia nina mambo mengi,akasema hunipendi,sikuhizi hunijali na blah!blah kibao. Tukaamua kuwa marafiki tu ila hapendi kuniona nikiwa na furaha hata kidogo wkt mm ni mcheshi na pia ni mhangaikaji.baada ya sikumoja akanambia kuamzia leo sitaki unipigie wala kunisms dah!niliumia sana ila kwa msaada wa marafiki zangu niliumia kama mwezi tu nakuvumilia hadi leo,nampenda sana huyo kaka ila ni mnyonyaji vibaya na pia ana mtoto ambae niilikuwa natoa msaada kwake lakini anatumia kuongea na simu sana,bado hajaajiriwa,wakuu samahani kwa kuikatisha network voda inasumbua sana.
 
Inaelekea alishakuchoka alikuwa anakutafutia kisababu

sidhani kama ni kweli maana nilionana na shem yaani kaka yake hakuamini kama naweza kuwa na mdogo wake yaani wote wako desperate about money
 
Duh! imeendelea....... pole mdada, kaka anakuletea ukoloni mamboleo huyo
 
Hadithi yangu imeisha......mpigieni makofi......
 
We umeelewa aliachwaje? au ndo umesoma kichwa cha habari tu, ukaconclude

By HARUFU

Inaelekea alishakuchoka alikuwa anakutafutia kisababu

Hii inatoa picha ya kwamba unapoomba ushauri, maneno utakayoambiwa uchanganye na akili zako..Mtoa post wala hajamalizia tayari conclusion ishatoka...hatari hii
 
Nakutogagwa! oli mulungi!

dadeki, haya mapenzi ya dar es salaam haya!

mwaanzia mapenzi ubungo mwaachania rangi 3!
 
sidhani kama ni kweli maana nilionana na shem yaani kaka yake hakuamini kama naweza kuwa na mdogo wake yaani wote wako desperate about money

Bora umemuacha, japo kakupa makovu moyoni lakini ni vyema kukimbia mapenzi yasiyo na future...
...sasa utulie basi sista, usiparamie mtu hadi akili ikae sawa, ukiweza fuata njia nzuri za kupata rafiki hadi uchumba na hatimaye ndoa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…