Niliachana naye mara nne lakini amerudi tena anaomba msamaha

Hacon

Member
Nov 13, 2015
63
23
Habari zenu wanaJF,

Natumaini ninyi ni wazima wa afya,

Ndugu yenu nimepatwa na shida kidogo kwa sababu sjui cha kuamua juu ya huyu mwanamke. Niliachana naye ni miezi 3 imepita walakini tulishaachanaga huko nyuma kama mara 4 hivi lakini ugomvi wa mwisho alimpigia rafiki yangu na kumwambia hatokuja kurudi kwangu tena labda kaburini na tatizo lilikuwa ni mimi kumwambia asitake kunipelekesha kwa sababu anataka ufanye anachotaka yeye na wala hatofanya wewe ambacho unataka, ni pasua kichwa.

Sasa jana kantafuta, ametoka hospitali alkuwa amelazwa akanitafuta na namba mpya na kunipigia akisema nanukuu "mume wangu kipenzi, nimekumiss sana, mimi mkeo umpendaye". Kwa sababu najua sauti yake haikunipa shida, tatizo limekuja sasa hivi anadai anataka kurudi kwangu huko alikokwenda ameona hana mapenzi ya dhati, moyo wake uko kwangu sio kwa mwanaume mwingine.

So nilikuwa naomba ushauri wenu nifanyaje maana ndiyo nampenda ila ni pasua kichwa.
 
Kaka huyu hana nia nzuri. Alaf ukiona dalili za kuachana achana kwenye mahusiano si nzuri kabisa.
Huyu dada kwanza hana msimamo... cha pili amekosa adab.. hakuheshimu.
Kwa haya uliyoeleza.. hafai.
Mwambie arud huko huko .. maana aliondoka mwenyewa tena kwa nyodo.
 
c6bf5c79bf06d3aaf1945a6eb848940e.jpg
 
Kaka huyu hana nia nzuri. Alaf ukiona dalili za kuachana achana kwenye mahusiano si nzuri kabisa.
Huyu dada kwanza hana msimamo... cha pili amekosa adab.. hakuheshimu.
Kwa haya uliyoeleza.. hafai.
Mwambie arud huko huko .. maana aliondoka mwenyewa tena kwa nyodo.
Asante bro 4 th advice
 
Back
Top Bottom