Niko njia panda, naomba ushauri

B'REAL

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2010
Posts
4,582
Reaction score
3,272
WAKU HABARI ZA SAHIZI.NAZANI WOTE MNAENDELEA VIZURI NA RAMADHANI KWA WALE WALIOFUNGA.WAKUU LEO MKUSHI KUNA JAMBO LINANITATIZA NIKAONA NI PATE USHAURI KIDOGO KUTOKA KWENU NIKICHANGANYA NA WAKWANGU NTAPATA UWAMUZI SA HII.

Ni kastory karefu kidogo ila ntaweka kwa ufupi, Miaka kama kumi na mbili iliyopita nilitokea kumpenda binti mmoja sana.

Na kila mtu alijua tunapendana kwani tulipita matatizo mengi pamoja.Tukaja tukapotezana kwa muda mrefu sana.

Huyo mwanamke alikuwa na rafiki yake kipenzi basi miaka ikaenda na yeye tukawa tumepotezana ila miaka miwili nyuma huyu rafiki yake akanitafta.

Mimi nilikuwa Arusha yeye Dar,basi katika zile siku akaja Arusha kwa ndugu zake,story story mara giza tukalala pamoja,kuazia siku hiyo tukawa wapenzi japo yeye mwenyewe anajua kiasi gani na mpenda rafiki yake kwa miaka yote hiyo ambayo sijaonana nae.


Basi ikapita mwaka hamadi demu akapata ujauzito na hakuniambia mpaka ilipokuwa imekuwa kubwa,japo sikuwa ndo plan zangu basi tukawa tunaishi hivyo Yeye anakaa kwao.

Basi siku zikawa zinaenda mwezangu ana lazimisha ndoa mi nikamwambia siko tayari bado kwa kufunga ndoa na pia kama anataka abadili dini liliweka icho kigezo kwa sababu sikuwa tayari kumuoa[cha udini] yote hii ni kwasababu sina feeling kumpenda sana japo ni mtu mkarimu anajali na anajua wajibu wake na anajitambua.

Kwa kweli namuonea huruma sana maana alisha zaa mtoto mmoja na wangu ni wa pili.

Sasa weekend hii yule mwanamke liliekuwa nampenda sana ambae ni rafiki yake tumewasiliana baada ya miaka kama kumi na mbili,ni baada ya kutafta kwa mda mrefu atimaye alikutana na rafiki yangu na kwa sababu rafiki yangu alikuwa anajua jinsi tulivyo akamuomba number ya simu akanipa, nimewasiliana nae na kutaka kujua yuko vipi?

Amesema ananipenda na hana mtu yuko single...

JE WA KUU NATAKA KUFUNGUA MOYO MAANA KIKWELI ILE TRUE LOVE NAISI NDO NINAYO MPENDA HUYU DADA YANI NAPENDA KIKWELI.

Yeye hajajua kama nimezaa na rafiki yake.

NIMEPANGA KUMWAMBIA UKWELI KABLA HAJAUSIKIA KWA MTU MWINGINE.

JE NTAKUWA NIMEFANYA SAHII KWA MDA HUU AU NISUBIRI?SIPATI PICHA YA REACTION ATAYO KUWA NAYO?

PILI JE KUHUSU HUYU RAFIKI YAKE NILIO ZAA NAE NIMWAMBIE UKWELI?WAKUU NIKO KWENYE HALI NGUMU SANA MAANA HUYU NILIE ZAA NAE NAMUONEA HURUMA.


 
Sasa hapo unapata kigugumizi gani? Ndoa inayojengwa juu ya uongo hujaa migogoro, weka mambo wazi na endelea na unayempenda ila kwa tahadhari, miaka 12 si mchezo.
 
Sasa kama unataka kua mzuri kote waoe wote,la unatakakile roho yako kinataka basi mweleze ukweli wewe ni mwanamme na sikuzote mwanamme anatakiwa awe na msimamo sio nataka sitaki au namuonea huruma, na jengine ivi kama kweli huyo rafiki wa alokua mpenzi wako ulishindwa kumwambia kama unamtafuta rafiki yake? au mda mloishi na huyu msichana wako wa mwanzo hakuwahi kukuonyesha hata kwa ndugu yake hata mmoja?
 
Funga safari mpaka aliko huyo kipenzi chako ukaungame hiyo dhambi ya kuzaa na rafikiye kama atakuelewa na kukubali muanze upya sawa maana naye lazima ana madhambi yake huko hata kama hayahusishi rafikizo maana miaka 12 ni uhai wa mtu!!!
Huyu uliyezaa naye sikushauri umuoe maana umekiri kuwa humpendi ila unamhurumia tu,lea mtoto na ukiweza msaidie financially aweze kusimama kwa miguu yake.
Kila la kheri!!!
 
Tatizo la wanaume hawana mcmamo....mwanamke anaweza kuamua jmbo moja asibadilishe..lkn mwanaume huamua hata mara 5...
 
Duh wengine tunatofautiana. Mtu mmepotezana miaka kumi na mbili na bado una hisia nae na unategemea may be kuja kuanza maisha nae
Duh pagumu hapo aise
 
mkuu achana na historia now u have a baby focus tu.... ila huwa mnapo pump bila kutumia kuziba mnategemea nini?
 
ni kweli mpenzi ni tatizo
miss chagga tunatofautiana sana kwa kweli miaka 12 na bado unasema mapenzi yapo
Miaka hiyo 12 je wewe mwanaume ushakuwa na wangapi ambao ulipita nao na huyo mwanamke alikuwa sister miaka hiyo kumi na mbili akiishi tuu anakusubiri aje akutafute akupate ndo muanze tena mipango
Na Kweli unaweza kutuminisha hapa kuwa miaka yote kumi na mbili mawazo yako na hisia zako zilikuwa kwa huyo dada zikisubiri apatikane mje muendeleze pale mlipoishia
Mkuu ushapata mtoto na huyo dada hebu lea mwanao na ujipange
Jenga hisia kuwa huyu ni mama mtoto wangu na achana kuwaza ndoto za alnacha za kuota ukiwa unatembea
 
Last edited by a moderator:
 
Jogoo kichaa kudadadeki unakimbiza mtetea hadi anajikwaa....
 
Hapo kama nakuona unataka vyote na utawakosa wote we jishauee then utajua mtakamawili mwisho ni nini?Huku unajifanya baba huruma kule true love.
Ushauri kama sio ustadhi ubadili dini uwaweke ndani Bi mkubwa na Bi mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…