Niko njia panda mwenzenu, nisaidieni tafadhali.

asante mkuu kwa ushauri wako ntaufanyia kazi.
 
Huyu jamaa mwenyewe hajapevuka kisawasawa na sidhani kama anastahili hata kuoa. "Kwa mtazamo wangu lakini" kuoa sio kuchagua ..nimuoe huyu au wa form six... Kama unavyofanya. Kuoa ni kufahamu tofauti ya ICE CREAM na UGALI... Kwanza kwanini uliamua kuwa na mwanamke mwingine wakati bado ulikuwa wangoja majibu ya kupendwa?? Na kwanini huyo amechelewa kukujibu??? Kwanini umuache uliyenaye?? Hana moyo wa nyama kwamba anaweza kuumia au ni changudoa ulimwokota so anytime unaweza kumwacha??? Jiulize kwanza kabla ya kufanya maamuzi hasa ya kuoa wazee wanasema fanya makosa yote sio kuoa, na fanya hima atleast uwe unamfahamu unaye taka kumuoa. Sio kuchagua kama mkate. Atakuzalia mtoto ndipo uanze kuona maajabu ya musa kama sio ya firauni.
 
wewe unampenda nani maana inaonekana uliyenaye unampotezea muda wake tu
kiukwei nampenda zaidi huyo mwanafunzi pia najiskia vibaya kama nikimwacha huyu nienae, roho inanisuta kwani nae ananipenda sana.
 
asante mkuu kwa ushauri wako ntaufanyia kazi.

Nitafurahi kama utarejesha majibu hapa jinsi umefanyia shauri zetu hapa kazi!! Si mnaleta tu mambo hapa tunapoteza energy kuwapa mawazo halafu mnaishia mitini bila mrejesho.
 
kiukwei nampenda zaidi huyo mwanafunzi pia najiskia vibaya kama nikimwacha huyu nienae, roho inanisuta kwani nae ananipenda sana.

Mpaka tuoe tunakuwa tumependa wanawake wengi na wengine kufikia hatua ya kuwa wapenzi!! Mwisho wa siku unaamua unaoa mmoja!! Na kwa uzoefu wangu wakati tunafikia kuoa huwa tunakuwa na watu wa kuwapima haswa!! Ni kweli kwa wanaume wengi na wanadada wa hapa mjue hivyo!! Last card inaamuliwa kwa kulinganisha!! So make uamuzi mapema usilete ubishi hapa!! It is simple!! Huna any commitment na huyo wa sasa!! Umeshasema unampenda zaidi mwanafunzi so kwa nini uaendelea kutuuliza hapa? Move one!! We once make decissions!! na kufunga vitabu.
 
 

Nimegundua kwamba wewe unataka msichanana akubebe ujauzito ile umridhishe mama yako na urudishe heshima yako kama kaka. Bali hujawa tayari kubeba majukumu ya familia. Ninavyojua hizo shule maarufu huchukua wanafunzi wenye umri mdogo, kwa hiyo hata huyo binti hajui madhar ya kubebe ujauzito akiwa bado mdogo. Ninaposema mdogo namaanisha ana umri chini ya miaka 20. Umesema kwao ni familia bora, kwa uzoefu wangu, familia itamshinikiza atoe mimba ili kutochafua jina la familia, pia, ili aweze kuendelea na elimu vizuri huku akifuata dira ya familia. Tafakari kwa kina na kuchukua za kikubwa. Epuka ukoloni wa kifikra.
 
Nitafurahi kama utarejesha majibu hapa jinsi umefanyia shauri zetu hapa kazi!! Si mnaleta tu mambo hapa tunapoteza energy kuwapa mawazo halafu mnaishia mitini bila mrejesho.

Ucjali mkuu ntaleta marejesho hapa baada ya kukutana na huyo mwanafunz ana kwa ana nimsikilize kwa umakini zaidi, atarudi mwezi wa tatu.
 

Cjaleta ubishi mkuu, mapenz sametime yanachanganya, niko njian kuoa na ni mwaka huuhuu sasa huyu kaingilia ghafla wakati nilishajisahaulisha kuhusu kumuoa mara ghafla kaniambia yuko tayari wakati mm nlitegemea haya akimaliza chuo.
 

Kumwambia wazazi wananishnkiza nilitaka kujua kama yupo tayari kuja kuolewa na mm lakin hata hivyo hakujibu chochote aliishia kukasirika kwa cku kadhaa kisha anakua kawaida, kama ni mtoto ningeshakuanae cku nyingi ila cpendi familia ya kua na watoto wa nje ntakaezaanae ndio atakua mama watoto.
 
Mhh anatafuta ada ya chuo huyo.Chezea hivyo viumbe vipo kimaslahi zaidi ila yangu ndo hayo
ndugu umenena vilivyo maaana bodi sikuiz wanatoa kitu kinaitwa NO LOAN...hapo sasa ndo shughuli inakwenda...sasa back to the point..inamaana huyo binti alichukua kitu kama mwaka kuja kukubali ombi lako..duuhhh hata visa ya uingereza inaprocessiwa ndani ya siku 3 sembuse huyo tu...? halafu utatakaje kuacha kitu ulichonacho na kukifuata ambacho hauko nacho..unamuacha wa sasa hivi kwa msingi gani? unafahamu kwamba what goes around comes around? yani ukitambaaa...kwenye point hizo naamini hautafanya makosa...vitu vingine ni kupuuzia tu..una compromise life linaendelea tu...
 
Wakuu naomba niongezee kitu hapa leo nimeongea na dada yake ni mtani wangu sana ila hajui kama nipo karibu sana mdogowe, nikamuulizia huyo mdogowe akanjibu bado hajamaliza nikamtania akirudi shule ntamuoa kabla hajaenda chuo, akaniambia baba hatakubali anampenda sana na hataki awe kama dada yao alimaliza six na mimba ya miez mi3 akazaa ndo akaenda chuo, ila hapa nimehisi mdogo mtu kachukulia point hapa na pia kaniambia mama yao aliolewa baada ya kumaliza six na mimba ya miez mi4 lkn hakwenda chuo baba yao alimkataza. mawazo yenu yatanisaidia sana pindi akimaliza mitihani yake mwezi wa tatu nijue ntamaliza vp hii inshu.
 
Wakuu naomba niongezee kitu hapa leo nimeongea na dada yake ni mtani wangu sana ila hajui kama nipo karibu sana mdogowe, nikamuulizia huyo mdogowe akanjibu bado hajamaliza nikamtania akirudi shule ntamuoa kabla hajaenda chuo, akaniambia baba hatakubali anampenda sana na hataki awe kama dada yao alimaliza six na mimba ya miez mi3 akazaa ndo akaenda chuo, ila hapa nimehisi mdogo mtu kachukulia point hapa na pia kaniambia mama yao aliolewa baada ya kumaliza six na mimba ya miez mi4 lkn hakwenda chuo baba yao alimkataza. mawazo yenu yatanisaidia sana pindi akimaliza mitihani yake mwezi wa tatu nijue ntamaliza vp hii inshu.
 
mkuu mimi nishampotezea mda tu hadi kumwambia niko na mpenzi mwingine, nkajua nae kanpotezea, jana ndio kaniambia hivyo mpaka sasa siamini kama ni yeye amenimbia maneno hayo kwa jinsi ninvyomfahamu.

atakuharibia mahusiano yako na uliyenaye sasa na utajutia bure! Mbaya zaidi yeye ndo kwanza yuko kwenye adolesence .... she still have a long way to go
 

wewe umeshakiri kua unampenda huyo student n nt uliyenaye so muache uliyenaye umuoe huyo wa zamani , me naangalia nnayempenda if yupo available nami nipo available kwa nini niumize kichwa na nisiwe naye, ya nini kujikita mapenzini na usiyempenda kwa dhati wakati chaguo lako lipo na cjaona kasoro zozote za kibinadam alizonazo zaidi ya kujitunza binti wa watu.
 

Asante kwa ushauri wako mzuri, nitaufanyia kazi.
 
Wandugu nashukuruni sana kwa ushauri wenu mmesaidia kwa kiasi fulan kung'amua nichukue uamuzi gani. Nawaahidi ntakuja tena hapa kuwajuza maamuzi niliochukua pindi huyo mwanafunzi akimaliza paper na kurudi dar.
 
Yuko njiana panda hajui njia so hapa pita kushoto
nakushauri endelea nahuyo ulie naye kwa sasa dent atakupa mlolongo mrefu sana japo unampenda let her go,na uache kabisa mahusiano naye hata ya kirafiki coz italeta mgogoro upande wa pili,,,wanawake wako hivi anaweza akawa anakuona kila siku anakujua au hata unawasiliana naye kila siku lakini asikuonyeshe chochote ,,,ila ukishaanza uhusiano ukamwambia au hata akafaham kwa njia zake inakua tabu na atajifanya anakupenda ,,,,piga chini maneno hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…