Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Nakumbuka enzi zile nikiwa bado chalii mdogo tulienda sehemu fulani palipokuwa na ubwabwa wa shughuli. Basi tukajikusanya kama watoto watano hivi, kisha bonge la sinia la ubwabwa likatua.
Kabla hatujaanza kufanya mashambulizi, mwenzetu mmoja ambaye alikuwa ni baunsa kuliko siye akatupiga biti, akatenga ubwabwa nusu sinia huku akisema, "asiyejipenda atie mkono huku!". Kama haitoshi, mbabe yule kwa jina la Kurwa alichukua achali kisha akaitapakaza kwenye ubwabwa wake wote akidhani ni kachumbari.
Weee, ile jamaa kupiga finga ya kwanza na kuisunda mdomoni tu, pilipili ilimuwasha mpaka akahisi mdomo unawaka moto. Kurwa akaona isiwe shida akakimbilia bombani kusuuza ulimi wake na hatukumuona tena!