Nikijikuna nina vimba

Mr Mayunga

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
313
40
Niliagizwa kutumia piriton,coz kila nilijikuna hua natoka uvimbe haswa maeneo ya tumbo,mapajani na miguuni.Kwa matibabu zaidi naomba ushauri wenu.
 
nakushauri uende hospitali ukaonane na wataalam kama utabahatika kuwapata maana huu mgomo si mchezo!

pia unaweza kutumia citrizen wakati huu ukiwa bado hujafika huko!
 
pole ndugu yangu una tatizo kama langu ,pana vitu viwili una alage ya chakula flani unapokula ,ama hali hewa joto ama baridi unapo oga maji ,kuna vidonge ukitumia unapata kupona kwa muda ,tafiti ktk vyakula ujue ni kipi ukila kinatokeza alage
 
Hiyo itakuwa ni alegi ya chakula fulani. Niliwahi kuwa na hali kama hiyo baada ya muda nikagundua kumbe nikila PWEZA ndo nawashwa na kuvimba. Nimeacha kula pweza na kuwashwa kuwetoweka.
 
Nenda hospitali ukapime. Uwezekano mkubwa ni kuwa una MINYOO. Kama huna basi una allergy ya kitu fulani labda chakula, nguo, mafuta, manukato, vumbi, baridi etc... Ni juu yako kutafuta hicho kitu mwenyewe. Itabidi utengeneze chati.
Anza na mafuta, sabuni, vumbi, baridi na manukato halafu nguo.
Malizia na chakula japo inaweza kukuchukua muda mrefu sana hata kabla hujagundua.
Kila la heri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom