Niki ukwaa URAIS... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niki ukwaa URAIS...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fiksiman, Jun 1, 2009.

 1. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kwa muda mrefu tumekuwa tukiwazodoa viongozi wetu kwa kile tunachokiita Ufisadi na ubadhilifu wa hali ya juu wa mali za umma. Tupo ambao tuko tayari hata kuingia mtaani kushinikiza kiongozi au mtu fulani aachie ngazi.

  Hii imenifanya nifikirie je nami niki ukwaa uongozi wenye hadhi kama urais au ubunge nitakuwaje, na haya ndo majibu yalikuja kichwani:

  1. Nitahakikisha naweka mjengo mmoja matata pale uswazi ambao utanilinda nikimaliza muda wangu. Huyo mjengo si wa kitoto, ikiwezekana uwe na hadhi ya 5 star hotel full kipupwe na nitajiunganisha maji moja kwa moja kutoka Ruvu mambo ya kutegemea Maji ya Dawasa na vijiankara nisahau kabisa

  2. Nitahakikisha hakuna ndugu anayekaa bure, kama hana elimu ya kutosha nitampeleka kusoma kwa gharama za serikali, wale wenye elimu zao nitawapa nafasi za ukurugenzi kwenye vitengo kama utalii, bandari na kwingine ambako hakuta kuwa na makelele ya walala hoi na waandishi

  3. Ishu yoyote ya manunuzi na tenda lazima ipitie kwangu ili kama kuna uwezekano ten percent iwe yangu...ni marufuku kuagiza vifaa vya serikali kama magari bila idhini yangu.

  4. Pia nitahakikisha nagusa nchi zote hapa duniani labda kuwe na vita. Nitaanza na Marekani, uingereza, Uingereza, Ufaransa (tena nasikia hawa wako fit sana kwenye majamboz) nitaonja totoz ya kizungu then Naelekea mashariki ya mbali yaani ni mwendo wa Emirates hadi Falme za kiaarabu then naomba pande la toto la kiarabu naunganisha familia kabisa.

  5. Suala la kuongoza nchi ntawaachia wasaidizi wangu mawaziri na hata kama kuna wapiga kelele wachache wataongea basi nitaweka kasuku mmoja pale ikulu ili awajibu hao wanoko.

  6. Nitawekeza japo kajumba kamoja ka biashara pale karibu na mbuga za wanyama na sio hata nikawa na viwili vya kupumzikia wakati wa retirement si unajua kuna vyeo vingine ukimaliza muda wako unakosa hata marafiki wa kukupa dei waka...we fikiria Rais mstaafu ataajiri kwenye kampuni gani hapa bongo labda upate shavu na UN la kusuluhisha migogoro na nina uhakika tunakoelekea vita itaisha na marais wengi watawahi kufa mapema.

  Anyway, yapo mengi ningeweza kufanya na nawashauri hata nyinyi mnaotia unoko muache maana hata mkipewa nyinyi sijui kama mtafanya tofauti na wale walio sasa.
   
 2. M

  Maquiseone Member

  #2
  Jun 1, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli wewe ni Fiksiman!!!!!!
  Kazi kwelikweli:'*&@#$%^
   
 3. s

  skasuku Senior Member

  #3
  Jun 1, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  And mind you guys.. this chap aint joking.... sio lazima mtu atembee uchi ili ujue ni kichaa....
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Naona utakufa kwa ulafi kabla ya kumaliza muda wa utawala wako!!!
   
 5. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Wewe bila shaka hautofautiani na mtazamo wangu, Je ungekuwa wewe ungefanya lipi la maana tuambie si kuponda wenzenu tu.
   
Loading...