Nigusie tamthilia zetu za panguso, tandi na shilingi - 2

Story Room

Member
Nov 27, 2020
56
147
Na mimi Sultan Uwezo.
Ninapoizungumzia FILAMU YA NYARA siyo kwamba nimeiandaa mimi la hasha bali nimejaribu kuangalia utofauti uliopo kati yake na nyingine ambazo ambazo mhusika ni MASIKINI anayeishi kwenye jumba bovu huko kijijini lakini angalia nywele zake, hata mavazi yake utapigwa butwaa, mtu ni chizi lakini kuuvaa ule uhusika kabisa hakuna mtu yuko jalalani lakini nguo zake Safi kajipiga mikwaruzo myeusi mikononi, miguuni na usoni. Kwanini mtu asiuvae UHUSIKA HALISI hata kwa asilimia SABINI tu, na ndiyo tunasema inawezekana tatizo ni MITAJI. Haya tukiiacha hii NYARA kuna nyingine ambayo najua wengi mmeiona inaitwa NYAMPALA mpaka mtu unajiuliza hivi hawa ni WABONGO kweli au wameongea KISWAHILI TU, watu wameuvaa uhusika mpaka unaogopa. TANDI ni series nzuri SHIDA imejaa wanaojiita NYOTA wengi ndiyo maana ikaharibu radha, SHILINGI nayo ni nzuri sana lakini ina makosa tuliyoyazungumza na inabebwa na WENYE PESA TU, PANGUSO ya Bwana JIMMY MAFUFU inakimbiza tatizo ni kupoa tofauti na awali huku muongozaji akijaribu kutafuta VISTORI vya kuisogeza mwisho. Nikiiangalia TAMTHILIA ya SINGLE MAMA ya mkubwa JB ilikuwa nzuri kwa kuwa iligusa jamii moja kwa moja alichokuja kuharibu ni namna alivyoimaliza inawezekana UHAI WAKE KWENYE TV aliukadiria akajikuta muda umefika lakini STORY bado ya moto, hivyo akasitisha na ndiyo kinachowaumiza hata wengine itakuwaje MWISHONI?


KWA LEO INATOSHA.
Edwin Soloma (Sultan Uwezo)
Instagram:mad:sultanuwezo_
Fb: Sultan Uwezo
Fb Page: TUNGO ZA SULTAN UWEZO
nyaramovie-___CIi72J0JNQb___-.jpg
IMG_20201221_193525_711.jpg
IMG_20201220_115412_822.jpg
 
tukienda nauhalisia hapa bongo kuna mishe mishe za kuteka watu na kumiliki silaha na kukimbizana kwa kuruka maghorofa?
 
Back
Top Bottom