Nigusie mbinu kadhaa za ufugaji wa kuku bora

Martin Mhina

Senior Member
Jul 24, 2013
169
37
(A) JINSI YA KUTENGENEZA MCHWA KWA YA KUPATA PROTINI YA ZIADA fuata hatua zifuatazo

1:Changanya kinyesi kikavu cha ngo'mbe na majni makavu / Mabua ya mahindi/Maranda ya mbao

2:Mwagia maji mpaka mchanganyiko ulowane

3:pakia/Weka kwenye chungu au boxes kisha uelekeze sehemu yenye dalili ya mchwa au kwenye kichuguu

4:Funika kwa muda wa masaa 25 baada ya muda huwo mcha watakuwepo wengi chukua box lako kamwage kwenye Kuku husaidia Sana ktk ukuaji
(B)KUTENGENEZA MINYOO YA CHAKULA (Red Worms planning ) Red worms planning ni utaratibu Wa kuzalisha minyoo kwa ajili ya kuku na Samaki, Zipo hybrid Red Worms Ambazo mara nyingi hununua sample kutoka nje ya nchi Kama Kenya,China au hapa Tanzania fuata hatua zifuatazo kuzalisha Red worms Asilia

1:(a)Chukua mavi ya ngombe mapya au ngombe aliyechinjwa mavi ya tumboni
:(b)Kusanya Damu damu, ngozi, utumbo, magoroto, nyamanyama nk

2:pakia kwenye kiloba au gunia kati ya ya choice A au B above

3:Chimba shimo la wastan kisha mwagia maji ndoo kubwa 4

4:Fukia hilo gunia na mwaga maji ndo 2 mara 1/2 kwa siku kwa muda wa siku 8/12

5:Baada Ya siku hizo kupita fukua na chepe utakuta minyoo mitupu ya kutosha kwa ajili ya Chakula cha Kuku au samaki na siku zinavyozidi kwenda ndo wanazidi kuzaliana na kuwa wakubwa

(C)UFANISI WA UFUGAJI WA KUKU BORA HUTEGEMEANA na mambo yafuatayo

1:Ujenzi wa banda bora kwa kuzingatia vipimo sahihi

2:Uchaguzi Wa kuku wazaz wenye sifa nzur

3:Udhibiti na tiba za magonjwa mbalimbali kwa kuzingatia Ratiba sahihi za chanjo

4:Ulishaji bora kwa waakati na Chakula kiwe na viin lishe vyote

5:Uzingatiaji Wa usafi Wa banda na vyombo

(D)SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU

1:Liingize mwanga na hewa muda wote

2:Liwe Kavu daima

3:Liwe na nafasi ya kutosha kuanzia vipimo vya upana 3M na urefu 4/5M kuku wasibanane

4:Liwe la Gharama Nafuu lakin la kudumu unaweza ukatumia Mabanzi, mbao, mianzi, matofali katika ukuta na paa tumia Vigae, Bati na nyasi

5:Liielekeze kuzuia upepo na mvua pia kuzuia wanyam na wadudu hatari kwa Kuku

6:Liwe na nafasi ya kuweka vyombo vya Chakula na ndani kuwe na maranda, bembea, vichanja

7:Kuwe na Uzio mpana angalau mita 10*12 ili wapate mahala paa kuota joto

(E)ILI KUEPUKA VIFO VYA KUKU FANYA YAFUATAYO

1:Osha banda na vyombo kwa dawa kama V-RID kila baada ya miezi 3/6 ili kuua bacteria nk

2:Chanja kuku chanjo zifuatzo Mahepe (Mareks ) kuanzia siku Ya 1-3 ,Mdondo siku 3-7 utarudia siku Ya 21,Gumboro siku 14 na Ndui siku ya 28 NOTE chanjo zote hizi utarudia kila baada ya miezi 3

3: Wape Vitamin Kama Multivitamin, vitalstress au maji ya molasses Ya unga

4:Usafi Wa banda ni muhimu Epuka watu kuingia bandani ukiweza kuwe na mavazi maalumu kama Ovaloli, maganbut zitazo fuliwa kwa dawa maalumu kwa ajili ya mfanyakaz na wagen wanaotembelea

5:EPUKA MAADUI HAWA HATARI KWA MIFUGO KAMA NYOKA, KENGE, PAKA, PANYA, MMBWA, KICHECHE NK KWA KUTUMIA MBINU ZIFUATAZO

1:Mwaga mafuta ya Dizel pamoja na mchanga zunguushia pembeni ya banda nyoka na kenge hatosogea

2:Chemsha mayai kisha yatege mahali Kuanzia mbwa, paka, nyoka, kenge, kicheche, akimeza lazima afe maana yai halitavunjika

3:Chimba shimo refu kidogo pemben ya kibanda au katikati kisha weka pumba, panya, mende, paka wamedumbukia ukiongeza na dagaa kidogo

4:ZUNGUUSHIA UA WA MTI WA NNYOKA (Mnyonga pembe )KAMA UZIO WA BANDA AU SHAMBA LA MIFUGO PEMBENI KWENYE MIPIKA, Mtii huu harufu yake hufukuza na kudhibiti KENGE NA NYOKA hata mwizi akitaka kuiba huwa mashaka ya kukamatwa pia mtii huu Majani yake /Magome yake yakipondwa.

Husaidia kuponya mtu aliyengatwa/kutemewa mate na nyoka Pia husaidia kuku aliye dumaa au mwenye minyoo kumboost Mtii huu hupandwa Kama muhogo Na unapatikana Tanga kwa wasambaa ndo niliuona NAAMINI MPAKA HAPA NIMEGUSIA BAADHI NA UMEPATA KITU FANYIA KAZI NA ULIZA UFUGAJI NI AJIRA NITAENDENDELEA
 
Huwo upo Tanga unapanda Kama Vigongo vya mihogo kuzunguuka banda au shamba una uweka na kuprune Kama Ua kuna kijana yuko kule kijijini korogwe nitamuuliza kama ataupata akutumie nitaweka your phone number here hata picha Kama utaujua utafute huko mkuu
 
Naomba kuuliza je chumba cha upana wa 3m x3m kinatosha kuku wangapi?
Kuku wakubwa ni wanne kwa mita moja ya mraba
Chumba chako 3x3m= 9 square meters. 9 X 4= kuku wakubwa 32

Kama ni vifaranga vya wiki 1 hadi 4, ni 16 hadi 20 kwa 1 meter square, so 9 ms inakuwa 9 X 16 or 20
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom