Nigeria yatolewa! Stars washindwe wenyewe tu!

MPUNGA

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
838
559
Kufuatia Nigeria kufungwa goli moja bila leo sasa wametolewa rasmi maana hata wakishinda mechi ya mwisho wataishia kupata pointi tano tu wakati MISRI wana pointi saba.

Kimahesabu ni Tanzania peke yake inaeweza inaweza kuito MISRI kama tutaifunga NIGERIA kwao na kuja kuwashughulikia waarabu mechi ya marudiano ambapo tunaweza fikisha pointi saba kama za MISRI. Issue itakuja kwenye uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.

HIVYO NI SAWA NA KUSEMA TIKETI YA STARS KWENDA AFCON ipo MIKONONI MWAO
 
sasa hv kundi la stars inaenda timu moja badala ya 2 nafasi bado ngumu hila nigeria sababu washapoteza wasitukomalie sana.
 
Wtanzania tudhamirie kufa na kupona kuifunga Misri bila kujali tutakwenda au la. Nafasi yetu kwenda mashindanoni ni ndogo mno lakni ni jambo zuri sana kujizoeza kuzifunga hizi timu kubwa. Ni mtaji mzuri huko mbeleni.
 
Ebu naomba kukumbushwa historia ya timu yetu ya Taifa Stars na timu za africa mashariki (waarabu):eek::eek::eek:
 
MNAPENDA UKWELI?
Basi tuuseme hepe tuache mapenzi. Hivi kweli mnaanza kutuaminisha tuwafunge Nigeria???????? Hivi kweli mnatauminisha tuwafunge waarabu??????? kwa ujuzi na uzoefu upi? mpira umekuwa siasa!! angalia wazairwaa pamoja na fujo zoote kwenye mpira no politic! wako wapi? vijana wetu wazuri sana , lakini mipango ni ya pwagu na pwaguziiiii
 
Hakuna sababu ya kujidanganya hapa, ukweli ni kwamba Misri tayari wameshafuzu kwenye kundi hili, Tanzania hatuwezi kuifunga Nigeria wala hatuwezi kuwafunga Misri.
 
h
Wtanzania tudhamirie kufa na kupona kuifunga Misri bila kujali tutakwenda au la. Nafasi yetu kwenda mashindanoni ni ndogo mno lakni ni jambo zuri sana kujizoeza kuzifunga hizi timu kubwa. Ni mtaji mzuri huko mbeleni.
hivi kinacheza kiwango au dhamira, acheni kuwatia watu pressure, waembieni hao wanaosimamia mpira wajenge kiwango na sio kuomba dua wakati miguuni mpira haukai, acheni kufikiria mambo hayo ya kuwashinda MISRI na Naigeria kwa kuomba dua.
 
Kumpenda mwanao ni jambo jema lakini mtoto wa jirani akiwa na uwezo mpe haki yake haya matumaini ya bandia tunayotaka yakite vichwani mwetu hayafai.Kweli mpira unadunda ila kiuhalisia tuangalie kiufundi kweli tunaweza kupambana na hizo timu mbili?tulishuhudia game na Algeria hapa kila mtu aliona mapungufu yetu achilia mbali sare tuliopata nyumbani na nigeria.Jamani mpira gharama tujenge kikosi cha kupambana hizi hadithi za paukwa pakawa hazitusaidii tunapenda timu yetu ila uwezo wetu bado.
 
...kwani TFF wameshaamua kuhusu upangaji wa matokeo ligi daraja la kwanza?!
....ili Tanzania isonge mbele,tunatakiwa kumfunga muarabu magoli 4-0,ili tuyazidi yale 3-0 waliyotufunga kwao.
....halafu tena,km itawezekana,japo inaweza isiwe lazima sana,ni vyema tumfunge Nigeria angalau 2-0 kwao,ili kumuondoa kabisa muarabu.Japo hata tukishinda 1-0 away kwa Nigeria, itakuwa poa kwetu.!
 
Kufuatia Nigeria kufungwa goli moja bila leo sasa wametolewa rasmi maana hata wakishinda mechi ya mwisho wataishia kupata pointi tano tu wakati MISRI wana pointi saba.

Kimahesabu ni Tanzania peke yake inaeweza inaweza kuito MISRI kama tutaifunga NIGERIA kwao na kuja kuwashughulikia waarabu mechi ya marudiano ambapo tunaweza fikisha pointi saba kama za MISRI. Issue itakuja kwenye uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.

HIVYO NI SAWA NA KUSEMA TIKETI YA STARS KWENDA AFCON ipo MIKONONI MWAO
Nigeria then Misri; Its an uphill task!!
 
Hizi timu kwa sasa hivi zinatisha kwa majina, na ndiyo sababu sasa Nigeria inayakosa mashindano ya AFCON kwa mara ya pili mfulululizo wakati Misri imeshayakosa mara tatu mfulululizo.

Kila zama zina mwanzo, na mwanzo ndiyo sasa ni kujiaminisha na kujipanga tu, wale NIGERIA mechi ya kwanza tuliwakosakosa kwa uzembe na papara zetu tu mechi ya marudiano hawatakuwa na motisha ya kujichosha wakati wameshatoka.

Tudhamirie ushindi tu, huwezi jua mbele ya safari kitatokea nini kama tulivyoshangazwa na CHAD. Soka la Africa haliishi kuwa na maajabu, fikiria Morroco ilivyojitoa dakika za mwisho kuandaa mashindano sababu ya ebola walivyokuja kufungiwa na nafasi kupewa Equatorial Guinea, au Ethiopia walivypokwa ushindi kwa kuchezesha mchezaji mwenye kadi michezo ya mwisho ya qualifiers.

Lengo liwe pointi saba hata kama tutatolewa kwa uwiano wa magoli, hiyo itakuwa ni chachu ya kufanya vizuri zaidi na kutujenga kiisakolojia kuwa tunaweza.
 
Yote yanawezekana,vijana wakaze misuli.
Kocha Mkwasa dhihirisha Dunia kwamba unaweza.
 
Maandalizi yaanze sasa ikiwa na mipango nje ya uwanja, waarabu hawa wakija kipindi cha joto kama sasa mechi ichezeshwe saa saba mchana kwenye jua kali la utosi, hapo hakuna kuomba poo ya kunywa maji, na ingefaa zaidi mechi inachezewa kama uwanja wa Mkwakwani 'jaruba la mpunga' kama unakidhi vigezo vya CAF, basi lao la kusafiri kwenda Tanga lipate pancha mara kumi na tano hata kama wakikodi wao wenyewe, wakiwa kwao hao ni watu dhulumati sana.
 
Back
Top Bottom