Kadi Poa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 2,015
- 1,005
Mahakama moja ya kijeshi nchini Nigeria imewahukumu kifo askari 54 kwa kukataa kupigana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram lililoteka maeneo mbalimbali nchini humo.
Wanajeshi hao ambao walipatikana na kosa la uasi, walituhumiwa kukataa kuikomboa miji mitatu iliyokuwa imetekwa na kundi la Boko Haram mwezi Agosti.
Wakili wa wanajeshi hao 54 alisema kuwa wanajeshi hao watauawa kwa kupigwa risasi huku wengine watano wakiachiliwa huru baada ya kukutwa hawana makosa.
Katika kujitetea wanajeshi hao wamelalamikia kuwa hawapewi silaha na mabomu ya kutosha kupigana na Boko Haramu ndio sababu ya wao kugoma kwenda kupigana.
Zaidi ya watu 2000 wameuwawa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi hilo hadi sasa na tayari maelfu zaidi ya watu wamelazimishwa kuhama makwao kutokana na vita vinavyoendelea.
Wakili aliyesimamia kesi hiyo Femi Falana, alisema kuwa wanajeshi hao wote walituhumiwa kupanga njama ya kuasi dhidi ya mamlaka ya kikosi cha Divisheni ya 7 cha jeshi ya Nigeria.
Wanajeshi wote walikataa mashtaka hayo na sasa hukumu hiyo inasubiri idhini ya Maafisa wa ngazi za juu wa Serikali hiyo kabla yakutekeleza adhma yao.