Nigeria kuchangia wanajeshi 200 kwenda Gambia

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Nigeria imethibitisha kuwa meli ya yake ya kivita inaelekea Gambia kama mazoezi wakati nchi za kanda zinajianda kuichukulia hatua za kijeshi Gambia.

Rais mteule Adama Barrow kwa saa yuko Senegal na anatarajiwa kuapishwa kesho, lakini Rais Yahya Jammeh anataka matokeo ya mwezi uliopita yafutwe na amekataa kuondoka madarakani.

Jana shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa mataifa ya magharibi mwa Afrika, yalikuwa yana andaa kikosi cha pamoja cha kuingilia kijeshi ikiwa Jammeh hataondoka madarakani.

Sasa shirika la habari la AP limemnukuu msemaji wa jeshi la wanamaji la Nigeria akisema kuwa jeshi la wanahewa la nchi yake linachangia wanajeshi 200 kwa kikosi hicho cha pamoja.

Chanzo: BBC
 
huyu dikteta wa Gambia sidhani kama anaakili timamu make angekua nazo hata kidogo angejiongeza, yaani nchi yako inamanajeshi 2500 tuu halafu unawaletea ubishi watu wanaotaka kuingiza wanajeshi karibia elfu3. si ni kutafta kudharirishwa tu na kusababishia maumivu wananchi wasokua na hatia. mambo mengine hayataki ujuaji achia ngazi umeshindwa halali basi
 
Uongozi ni dhamana. Pale mwanzo walimpa kura na kumchaguga Yahya. Sasa wamempa kura na kumchagua Adam. Kwanini Yahya aone shida kuachia madaraka wakati waliompa mwanzo wamemnyang'anya na kumpa Adam kwa njia ya kura? Dhana ya kuchagukiwa kwa njia ya kura Afrika bado ni tatizo. Wapiga kuwa wahashimiwe maoni yako.
 
Kwa nini hao wanajeshi 200 wasiwapeleke huko msituni wakapambane na Boko Haram? Hivi unaanzaje kumuone huruma ya njaa jirani yako ilhali nyumbani kwako kuna kwashakoo?
 
Back
Top Bottom