Nigeria-Boko Haram wafanya mauaji

Nigeria-Boko Haram wafanya mauaji

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,715
Reaction score
59,242
140604024332_borno_2_512x288_bbc.jpg

borno iliyoshambuliwa NIgeria


BBC imepata taarifa kuwa zaidi ya watu 20 wameuawa katika mashambulio katika vijiji vya jimbo la Borno.
Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi hilo yapata siku 50 zilizopita.


Wakaazi wa kijiji cha Attagara karibu zaidi na mpaka wa Cameroon na Nigeria wamesema kuwa watu waliovalia sare za kijeshi walikuja katika kijiji chao na kuwaagiza watu waje katika uwanja wa kanisa.


Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Mbunge wa eneo hilo Peter Biye amethibitishia BBC tukio hilo na kusema kuwa watu wengi wameuawa na nyumba kuchomwa katika vijiji vingine 5 mbali na hicho.


'Jeshi lakanusha madai'
Wakati huo huo jeshi la Nigeria limekanusha madai katika vyombo vya habari kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo imewapata na hatia baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi kwa kuwasaidia wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji kutoka jeshi hilo amekanusha madai kuwa kuna majenerali 15 wa wa jeshi waliofunguliwa mashtaka ya kuwasaidia magaidi.
Jeshi limesema kuwa taarifa hizo ni batili zilizolenga kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo wakati mambo yako tete.
140514153924_burnt_shops_borno_state_nigeria_512x288_afp.jpg

nyumba zimechomwa Borno


Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi wa maeneo mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio yaliyochacha.
Wapiganaji wamekuwa wakishambulia kwa bomu maeneo ya umma na kuwaua watu zaidi ya 200 katika chini ya miezi miwili tu.


Suala la wasichana waliotekwa pia bado limekaa kama mwiba wa samaki kooni mwa serikali ya Nigeria ambapo shinikizo kutoka jamii ya kimataifa zinaendelea kutaka wakombolewe kwa haraka.
Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kutokana na tisho la usalama lakini ssa polisi wametangaza kuwa maandamano ya amani yanaweza kufanywa.

Chanzo:BBC
 
Aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman
Nalilia amani......!!
Tui2nze bongo ye2 jamani..!!
 
Aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman aman
Nalilia amani......!!
Tui2nze bongo ye2 jamani..!!

Kama hawa magamba watalazimisha muundo wa muungano wa serikali mbili na kudharau maoni ya rasimu iliyopendekeza muundo wa muungano wa serikali tatu; ujue hayo mambo kama ya BOKO HARAM yanaweza kutokea hapa kwetu na hasa visiwani na baadae bara!!!
 
Hivi hawa Boko Haram wanataka nini haswa.
 
Back
Top Bottom