Niger yasitisha rasmi ushirikiano wake na Marekani

2 of Amerikaz most wanted

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
1,328
3,691
Niger has officially denounced Niger’s republic military cooperation with the United States of America 🇺🇸 with immediate effect.

It means that the USA air bases in Niger 🇳🇪 have been closed down and all USA military personnel in Niger have been ordered to leave Niger immediately.


IMG_20240317_145817.jpg
IMG_20240317_145844.jpg



Source African hub
 
Naam, Africa tumeanza kuamka.

Uwepo wa foreign military bases kwenye ardhi ya nchi yako ni fedheha, inakutia aibu
Kuna tabia moja hivi hawa wenzetu wanayo ambayo huitwa "condescending", si tabia njema sana kwa ulimwengu wa sasa.

Wamekuwa wakiwakalia kooni Niger na kuwalazimisha kuchagua washirika wakati Niger ni nchi huru yenye uwezo wa kujiamulia mambo yake.

Marekani bado yafanya mambo yake huku imeziba macho kwa pazia (blinders on) na wamesahau shida za kidiplomasia wanozipata katika maeneo ndizo zinosababisha ugumu wa diplomasia yake kwa bara la Afrika kwa sasa.

Ndo maana hata Tanzania yapaswa kuangalia sana misaada kama mchele ina malengo yepi khasa.
 
Naona wanawachokoza wazee wa fitina na unafiki, ngojea US ni awanyooshe.Juzi hapo Iraq walimwambia atoe majeshi yake,mkuu wa majeshi kawambia hawezi kutoa wanajeshi wake kwani anawasaka IS.

Hapo US anamtoa rais anamweka wake na anarudi tena.Ila siku hizi kwa kifupi US washamchoka, juzi Malaysia alileta hoja kwenye baraza la ulinzi la UN ya kuanza kuidiscuss kura ya Veto,wanataka iondolewe kwani US anaitumia vibaya.
 
We jamaa bana,unadhani kwa nini Niger,Mali,car,Chad hazitulii!?.. ufaransa alikua anavuna uranium inayoendesha mitambo yake ya umeme kwake,Sasa hivi ananua urusi,hizo nchi Zina uranium,gas,dhahabu,60% ya umeme wa France ulitokana na uranium ya niger
Sasa atayala Uranium baada ya kuwafukuza France? Wakae nae meza moja waweke mkataba vizuri then anakuwa mteja wa kudumu.
Sema kwavile hatujui ya nyuma ya pazia, ukute Rais anamfukuza France alafu analeta kampuni yake kufanya hiyo kazi na kuiuzia France tena kwa bei ya chini...Duniani kuna figure sana.
 
Sasa atayala Uranium baada ya kuwafukuza France? Wakae nae meza moja waweke mkataba vizuri then anakuwa mteja wa kudumu.
Sema kwavile hatujui ya nyuma ya pazia, ukute Rais anamfukuza France alafu analeta kampuni yake kufanya hiyo kazi na kuiuzia France tena kwa bei ya chini...Duniani kuna figure sana.
Acha ujinga
 
Back
Top Bottom