Heshima kwenu wadau,
Mwaka 1990 marehemu baba yangu aliamua kuoa mke wa pili. Miaka mitatu baadaye (1993) yule mke wa pili akafanikiwa kumhamisha kimapenzi baba yangu, akaamua kuondoka kabisa pale nyumbani. Mimi na wadogo zangu tumeishi maisha ya kutokumwona baba akitoa huduma yoyote kwetu toka wakati huo hadi kifo kilipomfika yeye na mkewe huyo wa pili mwaka 2011 kwa kukatwakatwa na majambazi kwa madai kwamba ni wachawi. Wameacha watoto watano. Mimi ndiye kijana pekee wa kiume mkubwa na ambaye ndiye pekee mwenye elimu ya Chuo Kikuu na uwezo kidogo kifedha. Mama yetu mzazi bado yupo hai. Toka 2011 ndugu zangu walitamani sana tuwatelekeze wale watoto wa yule mama wa kambo. Mimi nilikopa roho ya simba, nikaingilia kati. Nilimjengea nyumba mama yetu mzazi (70 yrs) na hao watoto walioachwa. Wanaishi pamoja japo kwa taabu sana. Kwenye uzao wa mama yetu mzazi sote ni watu wazima. Hakuna hata mmoja anayeishi karibu na mzazi wetu huyo. Tumemwekea mfanyakazi wa ndani kumsaidia huku hao watoto wote bado wanasoma.
Leo kinachonisukuma kuja kuomba msaada wa mawazo hapa ni: kila siku hao watoto wamekuwa wasumbufu kwa mama yetu. Wanamtukana, wanamsema vibaya na hata kumsingizia kuwa ndiye aliwaua wazazi wao. Kila msichana ninayempeleka pale, wanamtukana hadi anatoroka. Hivi ninavyoongea mama yangu anaishi bila msaidizi. Ninaumia kuona mama anapata shida. Ninaumia kuwaza kumwondoa pale mama maana tunaua mji wa urithi na watoto watakosa msaada. Ndugu zangu hawanielewi japo wananiheshimu kama mtoto wa kiume. Wnashauri niwatelekeze wale watoto kwa kumwondoa mama yetu. Nipo njia panda. Naomba ushauri wenu wadau.