NIDA wanauza nchi yetu kweupe kabisa

NIDA wanauza nchi yetu kweupe kabisa

Vitambulisho vipo vya aina mbili. Vya raia na wageni. Je alipewa kipi kati ya hivyo?

Hivi hawa kina NIDA, hivi vitambulisho wa Utaifa kwa nini vimechukua muda sana?

Na inaonekana ni kama hili halionekani kuwa tatizo! Kwa utafiti mdogo sana na wa kawaida, vitambulisho kama vya benki/ card za benki, hutengenezwa kwa muda mfupi sana! tena siku hizi vinakuwa tayari vimetengenezwa nawe unapewa tu siku unayojiunga na benki hiyo , hasa CRDB! hata passport au pasi za kusafiria, mbona hutengenezwa kwa haraka tu na aina ya taarifa tunazotoaga ni hizi hizi kama za vitambulisho vya Taifa, SASA TATIZO nini hasa, mimi nashindwa kabisa kuelewa, kwamba kuna nini hasa maalumu kinachohitajika ili kutengeneza kitambulisho cha Taifa? Pengine mimi sielewi mambo mengi juu ya mchakato huu, naomba kusaidiwa.
 
Mwalimu wako alikua na kazi sana,ni wapi kwenye uzi nimesema kapewa id. Kwakweli JF kuna mengi.

Hata kupiga picha hakuna maswali. Unataja jina wanatick unaenda kupiga picha. Hayo maswali yako wanauliza wakati wa kujaza fomu. Lete habari za ukweli uache upotoshaji. Kwani mzungu hawezi kua raia. Acha mawazo ya kitumwa.
 
Ubishi sio mtaji,hiyo ilikua inafanyika kwenye vituo vidogovidogo sasa hivi wamecentralize so fomu za watu ni nyingi.Leo kuna watu zaidi saba wamerudishwa na walishaingia kwenye chumba cha picha.Huwa si kurupuki ndugu.
 
Hivi hizi racist comments zinatokea wapi.. jamani saiv tupo 21st century .. ubaguzi wa rangi tushauzika karne nyuma huko.. sasa nyinyi mkiwa mnawabagua wakiwa huku tz alaf mna expect nn na nyie mkienda huko kwao.. come on grow up guys
 
Ndugu wanabodi leo nikiwa ofisi za mamlaka ya vitambulisho Kinondoni,nimeshuhudia mgeni akipigwa picha tayari kupatiwa kitambulisho.Aliletwa na Mtanzania na wala hakukaa kwenye foleni,alipofika kwa mpiga picha aliulizwa umeajiriwa? hakujibu ndipo afisa akauliza tena kwa kizungu cha ugoko "you employed? mzungu hakujibu,afisa mwingine mnene mweupe akambonyeza mwenziye aendelee na zoezi.Mzungu akafanikiwa akasepa huku akisindikizwa na wabongo wawili.Jamani NIDA waangaliwe vizuri.

MKuu kumbuka Kitambulisho cha TAIFA ni kwa ajili ya Kila MTu ata kama sio RAIA, ila tofauti ni kuwa cha SIO RAIA kitandikwa sio RAIA wa Tanzania.
 
Nadhani panahitajika elimu ya umma zaidi kuhusu vitambulisho vya taifa. Ninavyofahamu ni kuwa vitambulisho hivi vipi katika makundi kadhaa, ikiwa ni pamoja na raia wazawa wa Tanzania, wageni ambao wanapermanent resident permint n.k so kuna makundi mengi. Kwa kuwa kuwa tu ni mzungu aliyepewa haitoshi kusema tumeuza nchi au nchi imeuzwa, fanya uchunguzi zaidi uelewe huyo mzungu anafanya nini Tanzania, ukijua anafanya nini na je yupo Tanzania kihalali then tafuta ukweli je anahaki ya kupata kitambulisho na je amepewa category ipi ya kitambulisho? kuibuka tu na kusema hastahili kupewa kitambulisho unakosea, na hili ni tatizo kubwa kwa nchi yetu kwa sasa la kusema hovyo bila kufanya utafiti wa kutosha ili kujiridhisha na unachotaka watu wakipokee kutoka kwako. Pili kama kweli dhamira yako imejiridhisha huyo mzungu hastahili kupata hiyo hudumu wewe kama mtanzania mwenye uchungu na nchi yako ulichukua hatua gani? kuja kuandika JF na kuiacha hivyo? au ulitakiwa kuchukua hatua zaidi ili kufanikisha kuokoa nchi yako kuuzwa kwa watu wasiostahili. Polisi wanatoa namba za simu kila siku kwenye media mbalimbali ulipiga hata simu kuwa kuna huduma unahisi imetolewa kwa mtu ambaye umejiridhisha hastahili kupatiwa huduma hiyo? Nasema hivyo kwa sababu kama ni kweli hastahili tukio au kitendo hicho hakina tofauti na ujambazi ulitakiwa usaidie kufanikisha kuokoa nchi yako. Endapo umefanya hayo hongera ila kama umekimbilia kuongeza idadi ya post zako hapa JF basi hauna uzalendo wa kweli kama unavyotaka sisi tuamini.
Ndugu wanabodi leo nikiwa ofisi za mamlaka ya vitambulisho Kinondoni,nimeshuhudia mgeni akipigwa picha tayari kupatiwa kitambulisho.Aliletwa na Mtanzania na wala hakukaa kwenye foleni,alipofika kwa mpiga picha aliulizwa umeajiriwa? hakujibu ndipo afisa akauliza tena kwa kizungu cha ugoko "you employed? mzungu hakujibu,afisa mwingine mnene mweupe akambonyeza mwenziye aendelee na zoezi.Mzungu akafanikiwa akasepa huku akisindikizwa na wabongo wawili.Jamani NIDA waangaliwe vizuri.
 
Hivi hawa kina NIDA, hivi vitambulisho wa Utaifa kwa nini vimechukua muda sana?

Na inaonekana ni kama hili halionekani kuwa tatizo! Kwa utafiti mdogo sana na wa kawaida, vitambulisho kama vya benki/ card za benki, hutengenezwa kwa muda mfupi sana! tena siku hizi vinakuwa tayari vimetengenezwa nawe unapewa tu siku unayojiunga na benki hiyo , hasa CRDB! hata passport au pasi za kusafiria, mbona hutengenezwa kwa haraka tu na aina ya taarifa tunazotoaga ni hizi hizi kama za vitambulisho vya Taifa, SASA TATIZO nini hasa, mimi nashindwa kabisa kuelewa, kwamba kuna nini hasa maalumu kinachohitajika ili kutengeneza kitambulisho cha Taifa? Pengine mimi sielewi mambo mengi juu ya mchakato huu, naomba kusaidiwa.

Nikwambie tatizo..? Tatizo ni ujuha wa watanzania. Hawataki kuwachangamsha viongozi wao!
 
mleta ina maana haujui kuwa NIDA pia inatoa vitambulisho kwa wageni na wakimbizi wanaoishi kihalali hapa nchini??? kweli elimu bado inahitajika
 
Ubishi sio mtaji,hiyo ilikua inafanyika kwenye vituo vidogovidogo sasa hivi wamecentralize so fomu za watu ni nyingi.Leo kuna watu zaidi saba wamerudishwa na walishaingia kwenye chumba cha picha.Huwa si kurupuki ndugu.

ucha ubishi umekurupuka juha wewe
 
Nchi ngumu hii, mambo yote ni ujanja ujanja tu!!!

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
kinachoendelea NIDA ni kupiga deal tu,hakuna kitu cha maana pale zoezi gani ambalo haliishi watu hawataki zoezi liishe ili waendelee kupiga posho nchi hii imeoza ngoja tusubiri UFISADI MPYA kutoka NIDA si muda mrefu.muda wote Tz ni mzahamzaha,na mchezomchezo tu wala watu hawajali na wengine wanashabikia mchezo huu,haya ma dark continent tabu tupu.
 
waliopo ikulu wanakula vya ikulu, waliopo bungeni wanakula vya bungeni, waliopo wizarani wanakula vya wizarani. JE NAO WAKILA VYA NIDA KUNA UBAYA GANI?
 
Hivi kamati ya hesabu inaenda mini kukagua hesabu za NIDA ili nao wapate cha ncha Kali?
 
Back
Top Bottom