kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,190
- 24,620
Nikki Haley: 'Trump ni kichaa', ndiyo sera niliyotumia UN kufanikisha malengo ya Marekani
Balozi wa Marekani aliyejiuzulu, wa Umoja wa Mataifa amesema, ili kuweza kutwisha rai na mitazamo yake katika Baraza la Usalama la umoja huo, alikuwa kila mara akionyesha na kutaka iaminike kuwa Donald Trump ni mtu kichaa na mwenye mwenendo usiotabirika.
Akizungumza katika mahojiano na gazeti la The Atlantic linalochapishwa nchini Marekani, sambamba na kuteuliwa mfuatizi wake katika UN, Nikki Haley amesema, wakati wa majadiliano na mabalozi wenzake katika Baraza la Usalama, hususan katika kupitisha maazimio dhidi ya Korea Kaskazini, alikuwa akijaribu kuonyesha kuwa Rais Donald Trump wa Marekani ni mtu mwendawazimu, ili kuwaghilibu wanadiplomasia wenzake na kuwezesha kupitishwa maazimio yanayotakiwa na Washington.
Akijibu suali, vipi Russia na China ziliweza kushawishika na kuridhia mara tatu mtawalia kuwekewa vikwazo Korea Kaskazini, balozi huyo wa Marekani aliyejiuzulu amesema: "Nilikuwa kila mara nikieleza katika Baraza la Usalama kuwa, siwezi kujua Trump anaweza kuchukua hatua gani. Nikisema, mimi siwezi kumzuia, anaweza kuchukua hatua za kijeshi."
Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita wa 2017, baadhi ya duru za Marekani ziliripoti kuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump amewataka wasaidizi na watu wake wa karibu wamtaje yeye kwamba ni mtu "kichaa" ili wapate zaidi matakwa na matilaba yao katika mazungumzo.../