Nichukue uamuzi gani?

Dooh mkuu pole sana, inasikitisha sana.. Sijui hata nikupe uahauri gani lakini punguza jazba kidogo, usije kuchukua maamuza ambayo yatakugharimu baadae

Kama unampenda huyo binti basi mvumilie maana muda unavyoenda atapona hayo majeraha "time heals"

Kuhusu hao wazazi wake, wasamehe tu maisha yaendelee.
 
Asante mkuu kwa ushauri wako
 
umeshajaribu kumpeleka kwenye counseling? anahitaji sana sana kupewa counseling tukio la kubakwa huwa lina affect maisha ya mtu for the rest of her life, na hata kwenye tendo itakuwa shida kwenu hata kama utamvulimia mpaka ndoa lakini mwisho wa siku psychologically huyo mtu hayuko sawa mnaweza kuishia kuwa na ndoa isiyo na amani. Na kwa wewe wasamehe tu hao wazazi na huyo alietenda hicho kitu wala usitake kumjua mana unaweza jikuta umefanya jambo ambalo litagharim maisha yako. Ila she really really needs help
 
anahitaji ushaur tu wa kisaikolojia atakuwa sawa na utamgegeda vizur tu
 
wewe ni shujaa,,,,unaelekea ukomavu halisi....ushauri wangu,,,,maisha ya nyuma ukiyaweka mbele yako huwezi move broo.....futa delete tupa kule.....peleka posa....vuta kinu ndani......anzeni maisha upyaaaaaaa.....zingatia haya....hakikisha na yeye ameridhia,,,, sio kesho kushokutwa anaanza oooohhh nilikwambia nimebakwa hukunisaidia.....vigeu geu kweli hao.....kila la kheri....
 
anahitaji ushaur tu wa kisaikolojia atakuwa sawa na utamgegeda vizur tu
Nia yangu sio kumgegeda na ingekuwa hiyo labda ningeshamgegeda mara kibao au tungeshaacha. Nia yangu ni kuishi nae siku zote kwa furaha tuwe na watoto wetu, tufurahie maisha. Asante lwa mchango wako.
 
Huwa anapata counseling ila ni mara chache.. Nitajitahidi kuzungumza nae niona kama tunaweza kupata counseling regularly
 
Nitajitahidi mkuu, naomba kwa Mungu pia afanye wepesi
 
Pia msisahau kupima HIV
Vipimo vyote tumepima zaidi ya mara moja, yupo sawa kiafya hana shida na zamani alikua hali kabisa ana mawazo ila nimejitahidi siku hizi amekuwa tofauti hata kujichanganya na kutabasamu tofauti na kabla ya hapo
 
Anachohitaji sasa huyo binti ni hakikisho la usalama wake binafsi na upendo wake.
Kutafuta haki ni sawa lakini haibadilishi chochote zaidi ya kulipiza kisasi.
kama unampenda tangaza nia, fuata njia sahihi, oa kwa utaratibu unaokubalika ili umfanye kuwa na uhakika na uhalali wa mahusiano. kuzaa au kuishi kabla ya ndoa halali, utakuwa hauna tofauti na huyo mbakaji, kwa sababu unaweza kumtenda na hili likamharibu zaidi kisaikolojia!
Kama una mpenda, You are the cure!



 
Asante mkuu. Nitajitahidi kufanya hivyo.
 
MKUU AMETUMIA KIGEZO GANI KUKUPA MIEZI SABA?.KWANINI ISIWE MITANO ,ISIWE MOJA, NAULIZA HIV KWASABABU INAWEZA IKAFIKA MIEZI SABA IKAWA HAITOSHI KUMBE ILIBIDI MIAKA SABA.....
 
MKUU AMETUMIA KIGEZO GANI KUKUPA MIEZI SABA?.KWANINI ISIWE MITANO ,ISIWE MOJA, NAULIZA HIV KWASABABU INAWEZA IKAFIKA MIEZI SABA IKAWA HAITOSHI KUMBE ILIBIDI MIAKA SABA.....
Aliniambia nimpe miezi saba apone kabisa.. Sikuelewa sana ila sikutaka kumbishia kwakuwa nampenda kwa moyo na nimesha invest muda wangu mwingi kwake hivyo miezi saba kwangu sio mingi. Hofu niliyo nayo ni baada ya huo muda kutimia je hataibuka tena na sababu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…