Son Of Almighty
Senior Member
- Jun 28, 2017
- 133
- 451
Habari za Asubuhi Wakuu..
Ni miezi 10 sasa toka nidhulumiwe/ nitapeliwe 2mil na mtu ambaye nilimuamini sana na sikutaraji leo hii ingefikia hapa..
Nilifungua ofisi ambayo nilimuweka yeye kama msimamizi sababu ni kazi alokuwa na ujuzi na uzoefu nayo. Awali sikuwa na shaka naye ila baadae kupita miezi kama 3 na ofisi kuwa haileti pesa na saundi zikiwa nyingi nilimua kufanya uchunguzi na kubaini nimeibiwa sana zaidi ya mtaji niloweka kwa kazi ambazo tayari zilishafanyika kwenye ofisi yangu.
Baada ya kumbana mhusika alikiri na kuomba samahani na kuahidi kulipa; kuepusha nisiingie hasara zaidi basi kishingo upande na lengo ni pesa yangu irudi tuliandikishana mbele ya serikali ya mtaa kuwa pesa yangu arudishe tena pasipo riba kuepuka usumbufu na kelele na walimwengu.
Ndugu huyu alianza kuwa msumbufu sana, ikanibidi niripoti suala kwa ofisi ya RC na ikatoka barua kwenda eneo husika, basi akalipa theluthi ya deni na kuahidi kulipa inayobaki mwezi unaofuata, ajabu mpaka sasa ni miezi 4/5 hajalipa chochote na mbaya nimeshafika ofisi za wilaya husika napo walopewa jukumu la kusimamia suala langu nao imefikia wananikwepa; hawajibu msg wala kupokea simu zangu kabisa. Imefikia hatua hata nilipokwenda mara ya mwisho wanaonesha dharau za wazi kuhusu suala la kufuatilia haki yangu.
Yapata wiki 2 mdeni alipigiwa simu na ofisi ya mkoa baada ya kupeleka malalamiko yangu na akakiri na kusema ni kweli, akaomba alipe mwisho wa mwezi July ila ajabu alipopigiwa siku husika hakupokea kabisa, na ghafla hapatikani kabisa ila yupo na eneo alipo inajulikana.
Kila nikifikiria pesa yangu ilipotea zaidi muda wangu, pia dharau ambazo mdeni ananifanyia na wahusika serekali ya mtaa na mkoa pia hakika ninawaza kufanya maamuzi ambayo cjui nieleze vipi?
Naomba Ushauri hasa wataalamu wa sheria; walopitia scenario kama hizi na mwisho wakafanikiwa kupata haki zao, mimi ni mtu mwenye roho njema sana na kaliba ya huruma ila kwa hili nimeamua rasmi wacha tuonane wabaya tu. Kinachouma zaidi ni jinsi jamaa anavoniponda kwa dharau na kunichafua kwa kitu ambacho ni haki yangu.
Nakaribisha Ushauri au mwenye mawasiliano ya Waziri Jafo, anisaidie. Au kamanda wa takukuru ili nimmwagie huyu Afisa Tawala na DAS ugali na mboga kabisa