yello masai
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 3,922
- 4,181
Ni takiribani mwaka mmoja tangu nilipomuoa. Kabla ya hapo alikuwa akiishi na mama ake wa kambo.
Tangu nimemuoa huyu mke wangu mama ake huyu amekuwa kila mara akija kwangu [kama mara sita au 5] na mara nyingi anakuja analala.. Kiukweli hii inakuwa kero kwangu ukizingatia nimepanga chumba na sebule tu, so akija hulala sebuleni.
Yote hayo tuyaache. Sasa ni kwamba juzi alikuja na kaondoka jana, sasa leo asubuhi naenda kupiga mswaki nikatafuta dawa ya mswaki siioni, nilivyomuuliza mke wangu kama anajua ilipo akaniambia nilimpa mama kaondoka nayo.
Kiukweli nimepigwa butwaa, najiuliza dawa tuliyokuwa tunatumia inakuwaje ampe mama? Na wakati anajua kabisa ndani hakuna dawa nyingine.
Kiimani pia naliona hili haliko sawa.
Nipeni ushuri kwa hili wadau. Nichukue hatua kwa hili, na hatua gani?